Zaidi ya droni 100  zilionekana zikiruka sehemu tofauti za nchi, huku jeshi la anga likijaribu kudungua baadhi ya droni hizo. Miripuko pia iliripotiwa katika maeneo ya Cherkasy, Chernihiv, Dnipro na Kiev.

Hadi sasa hakuna taarifa za waliojeruhiwa au hasara iliyotokana na mashambulizi yaliyofanywa katika miji hiyo.

Hata hivyo kiongozi wa mji wa Zaporizhzhya Ivan Fedorov, amesema mashambulizi yaliyoshuhudiwa huko yaliwajeruhi watu watatu  huku majengo kadhaa yakichomwa moto.

Vyombo vya habari vya Ukraine vimetoa onyo kwa wakaazi kwamba huenda mashambulizi kama hayo ya anga, yakaendelea kushuhudiwa katika siku za hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *