#HABARI: Mahakama ya Mkoa wa Vuga, tarehe 27/08/2025 imemhukumu Mshtakiwa Nassor Seif Khamis (47) mkazi wa Nyerere Zanzibar, kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 13 jela kwa kosa la Unyang’anyi wa Kutumia silaha huku akijua kuwa, kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 25/01/2025 majira ya saa 03.00 usiku huko maeneo ya Fuoni Kibondeni Wilaya ya Magharibi B” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja ambapo mshtakiwa alitumia silaha kumnyang’anya mlalamikaji simu 03 zinazotumika kwa huduma ya miamala ya kifedha na fedha taslimu Milioni Ishirini na Moja (21,000,000/-Tsh) ambapo vyote vina thamani ya Shilingi za Kitanzania Milioni Ishirini na nane na laki tano na Elfe Hamsini (28,550,000/-Tsh)
Mshtakiwa alifanya kosa hilo ambalo ni kinyume na kifungu cha 280 cha sheria ya Adhabu 6/2018, Sheria ya Zanzibar.
Akisoma maelezo ya hukumu, Hakimu Mheshimiwa Haji Ibrahim, amesema mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na mashahidi saba (07) wa upande wa mashtaka ambao hauna chembe ya shaka na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.
Kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapo tarehe 28/04/2025 na kuanza na kupewa kesi namba 66/2025.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @radioonetanzania