
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Anicet-Georges Dologuele, ameamua kufuta uraia wake wa Ufaransa, ili kuwania urais katika nchi yake.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii inamaanisha kuwa, anajiandaa kumenyana na rais wa sasa Faustin Touadera, wakati uchaguzi huo utakapofanyika Desemba tarehe 28 mwaka huu.
Mwanasiasa huyo wa upinzani amesema, uamuzi aliuchukua ni binafsi, na kuitaka Tume ya uchaguzi kuhakikisha kuwa, uchaguzi huo unakuwa huru na haki.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Dologuele, kujaribu kutafuta uongozi wa nchi hiyo. Mwaka 2020 aliwania, na kumaliza katika nafasi ya pili, katika uchaguzi ambao ulidaiwa kugubikwa na wizi wa kura.
Wachambuzi wa siasa wanasema, hatua hii ya mwanasiasa huyo maarufu imesukumwa na kile ambacho wapinzani wa Touadera wanasema, unatokana na mpango wa kiongozi huyo kuwa na mpango wa kusalia madarakani kwa muda mrefu, baada ya kubadilisha katiba mwaka 2023 ili awanie muhula wa tatu.