#HABARI: Chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzania itaanza uchimbaji wa uranium katika Wilaya ya Namtumbo, Ruvuma, yenye akiba ya tani milioni 139 na uhai wa mgodi ni miaka 22.
Mradi huu una gharama ya shilingi trilioni 3.06 na unajumuisha uchimbaji na kuongeza thamani ya uranium ndani ya nchi, pamoja na mpango wa kuunda kiwanda cha nguvu kwa kutumia uranium kilichochimbwa hapa nchini.
Utekelezaji unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 4,000 za moja kwa moja na zaidi ya 100,000 zisizo za moja kwa moja, huku ukilenga sera ya serikali ya kuongeza thamani ya ndani kwenye Sekta ya madini.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania