#HABARI: Katika kuboresha utendaji kazi na usimamizi wa masuala ya mipango miji nchini, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya M…#HABARI: Katika kuboresha utendaji kazi na usimamizi wa masuala ya mipango miji nchini, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya M…

#HABARI: Katika kuboresha utendaji kazi na usimamizi wa masuala ya mipango miji nchini, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Idara ya Maendeleo ya Makazi inaendesha kikao kazi kwa Maafisa Mipango miji wa mikoa ili kujipanga kutekeleza majukumu yao kwa weledi.

Kikao hicho cha siku tatu kinachofanyika mkoani Arusha kuanzia Septemba 01, 2025 hadi Septemba 03, 2025 kinatumika kukumbushana maadili kwa Maafisa Mipango miji, muongozo wa upangaji na utekelezaji mipango ya uendelezaji miji, umuhimu wa kufanya ukaguzi wa matumizi ya ardhi pamoja na uidhinishwaji kazi za mipango miji kwenye mfumo wa e-ardhi.

Idara ya Maendeleo ya Makazi moja ya majukumu yake ni kupanga miji vizuri pamoja na kusimamia uendelezaji wake (Development control).

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Deogratias Kalimenze amewaambia washiriki wakati wa kufungua kikao hicho kuwa, Maafisa Mipango miji ndiyo waliobeba dhamana nzito ya kuhakikisha ulimwengu unakuwa na sehemu salama ya kuishi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa idara ya Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, upangaji wa miji ni jukumu ambalo watendaji hao wamepangiwa na Mwenyezi Mungu waweze kuilinda dunia na kuwa endelevu.

Kupitia kikao hicho, tathmini ya utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka 2024/2025 pamoja na utekelezaji kazi za urasimishaji nchini itafanyika.

Aidha, kutakuwa na uwasilishaji mada kuhusiana na mfumo wa utoaji huduma za Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango miji, kupitia na kujadili rasimu ya kanuni ya viwango vya upangaji na makundi ya matumizi pamoja na namna ya kulinda afya ya akili na umuhimu wa akili hisia katika maeneo ya kazi.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *