#HABARI: Mgombea Ubunge Jimbo la Bukene lililopo mkoani Tabora kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), @JohnLuhende, amesema akipata…#HABARI: Mgombea Ubunge Jimbo la Bukene lililopo mkoani Tabora kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), @JohnLuhende, amesema akipata…

#HABARI: Mgombea Ubunge Jimbo la Bukene lililopo mkoani Tabora kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), @JohnLuhende, amesema akipata nafasi ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo atahakikisha anaboresha miundombinu ya barabara, Afya, Elimu, Kilimo pamoja na umeme ili kufungamanisha sekta moja kwenda nyingine ili kukuza uchumi wa wananchi Jimbo hilo.

Luhende ameyasema hayo jana wakati anazindua Mkutano wa Kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge uliopo pembezoni mwa Ofisi ya CCM, Kata ya Bukene, huku akiwaomba wananchi wa Jimbo hilo waweze kumpa ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo ili kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi.

Luhende amewaomba wananchi wa Jimbo hilo kuchagua mgombea wa Urais kutoka chama hicho ambaye ni Dkt.Samia Suluhu Hassa, ili aweze kuendelea kuwa Rais wa Tanzania, lakini pia wamchague yeye kuiwa Mbunge pamoja na madiwani wa chama hicho ili kwa pamoja waweze kuboresha miundombinu na Maisha ya wakazi wa Jimbo hilo.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania #uchaguzimkuu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *