.

Chanzo cha picha, Getty Images

Msemaji wa kundi la wapiganaji la Hamas, Abu Obeida, ameuawa
katika shambulizi la anga katika mji wa Gaza, Israel imesema.

Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz alipongeza Jeshi
la Ulinzi la Israel (IDF) na shirika wa usalama wa Israel, Shin Bet, kwa
“utekelezaji sahihi” wa mauaji hayo kwenye ujumbe wake katika mtandao
wa X.

Hata hivyo, Hamas bado haijathibitisha kifo cha Abu
Obeida. Kundi la wapiganaji wa Palestina hapo awali lilisema makumi ya raia
waliuawa na kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya Israeli kwenye jengo la
makazi katika wilaya hiyo.

Waandishi wa
habari wa eneo hilo waliripoti kuwa takriban watu saba wameuawa na wengine 20
kujeruhiwa katika mashambulizi hayo katika kitongoji chenye wakazi wengi cha
al-Rimal katika mji wa Gaza, huku watoto wakiwa miongoni mwa waliojeruhiwa.

Shambulio
hilo la Jumamosi limetokea huku kukiwa na mashambulizi ya anga yanayoendelea
katika mji wa Gaza kabla ya mashambulizi yaliyopangwa na Israel.

Katz alionya
Jumapili kwamba wengi zaidi “walioshirikiana na Obeida katika uhalifu”
wangelengwa katika ” kampeni inayoendelea huko Gaza” – akirejelea
mpango ulioidhinishwa hivi karibuni wa Israeli wa kutwaa udhibiti wa jiji la
Gaza.

IDF na Shin
Bet walitoa maelezo zaidi kuhusu shambulizi la siku ya Jumamosi ambalo lililenga
msemaji wa Hamas.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *