Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wamekubaliana ada ya £125m na Newcastle kumsajili Alexander Isak. The Reds watawasilisha ada ya rekodi ya Uingereza itakayofikia £130m. (Telegraph)
Aston Villa wamefanya mazungumzo na Manchester United kuhusu usajili wa winga wa England Jadon Sancho, 25. (Athletic)
Aston Villa pia wamewasilisha nia ya kumsajili kipa wa Kibelgiji wa Royal Antwerp, Senne Lammens, 23. (Fabrizio Romano)
Bayern Munich wameondoa ofa yao kwa mshambuliaji wa Chelsea na Senegal Nicolas Jackson, 24. (Florian Plettenberg)
Tottenham wamewasiliana na Atalanta kuhusu usajili wa winga wa Nigeria Ademola Lookman, 27, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Bayern Munich. (Sky Sports Germany)
Chanzo cha picha, Getty Images
Galatasaray wako kwenye mazungumzo na Tottenham kuhusu dili la kumsajili kiungo wa Mali Yves Bissouma, 29. (Independent)
AC Milan wamewasilisha ofa rasmi ya kumsajili kiungo wa England wa Liverpool, Joe Gomez, 28, kwa mkataba wa kudumu, huku vilabu vikiwa kwenye mazungumzo. (Fabrizio Romano)
Fenerbahce wanataka kukamilisha dili la kumsajili kipa wa Brazil Ederson, 32, kutoka Manchester City baada ya wapinzani wao wa Uturuki Galatasaray kukataliwa ofa ya euro milioni 10 (£8.7m). (Fabrizio Romano)
Newcastle United wanataka kumsajili mshambuliaji wa Ukraine wa Roma Artem Dovbyk, 28, kwa mkopo wenye kipengele cha kumnunua moja kwa moja kwa ada ya £30m. (Sun)
Aston Villa wamekubaliana na Aberdeen kumsajili kiungo wa kati wa timu ya vijana ya Scotland Fletcher Boyd, 17. (Football Insider)
Kikosi cha Unai Emery, Aston Villa, pia kiko karibu kumsajili beki wa Kiswidi Victor Lindelof, 31, ambaye yupo huru baada ya kuondoka Manchester United mwishoni mwa mkataba wake. (Birmingham Live)