“Matendo ya wapenzi wa jinsi moja” sasa yamepigwa marufuku na kuharamishwa nchini Burkina Faso. Sheria inayoruhusu vifungo vya hadi miaka mitano jela imepitishwa siku ya Jumatatu, Septemba 1, na Bunge la Mpito kama sehemu ya marekebisho ya Kanuni ya Kibinafsi na Familia. Hadi sasa, hakuna sheria inayolenga wapenzi wa jinsia moja nchini Burkina Faso, ambao hata hivyo wanaishi kwa kujificha nchini humo. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rasimu hii mpya, ambayo bado haijaidhinishwa na kiongozi wa utawala wa kijeshi Ibrahim Traoré, pia inarekebisha masharti ya kupata uraia wa Burkina Faso na umri halali wa ndoa.

Nchini Burkina Faso, yeyote atakayepatikana na hatia ya ulawiti ataadhibiwa kwa kifungo cha miaka miwili hadi mitano jela na malipo ya faini, ameeleza Waziri wa Sheria Edasso Rodrigue Bayala kufuatia kupitishwa kwa kanuni hiyo mpya. “Kosa litakapojirudi, ikiwa mhusika sio raia wa Burkina Faso, atafukuzwa nchini,” ameongeza waziri huyo.

Mabadiliko mengine makubwa yanahusu umri halali wa ndoa. Imepunguzwa kutoka miaka 20 hadi 18 kwa wasichana na wavulana. Walakini, “msamaha maalum” wa miaka 16 unaweza kutolewa kwa ombi. Ndoa za kitamaduni na za kidini pia zitatambuliwa kisheria, mradi tu wanandoa watawasilisha ombi rasmi kwa ofisi ya sajili ya raia.

Suala la kumpa mtu uraia wa Burkina Faso pia limerekebishwa katika kanuni hii mpya ya familia ili kuzuia, kulingana na Waziri Edasso Rodrigue Bayala, ulaghai wa kihisia na kiakili. Sasa itachukua miaka mitano kupata uraia kupitia ndoa. Ikiwa mmoja wa wanandoa haishi Burkina Faso, kipindi hiki kinaongezeka hadi miaka saba.

Kuhusu waombaji wengine, kwanza watalazimika kupata kadi ya ukazi wa kudumu na kusubiri miaka kumi kabla ya kupata uraia wa Burkina Faso. Hata hivyo, mtu yeyote anayefanya vitendo kwa kushirikiana na raia wa Burkina Faso, wageni, au nchi ya kigeni, dhidi ya “maslahi ya Burkina Faso” atanyang’anywa uraia wake wa Burkina Faso.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *