
Nchini DRC, hatima ya kisheria ya waziri wa azamani wa sheria wa DRC Constant Mutamba itajulikana Jumanne, Septemba 2. Waziri huyo wa zamani wa Sheria, ambaye alilazimika kujiuzulu mwezi Juni, anashutumiwa kwa kujaribu kufuja karibu dola milioni 20. Mwendesha mashtaka ameomba miaka kumi ya kazi ngumu kwa ubadhirifu wa fedha za umma.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Paulina Zidi
Nchini DRC, hukumu iliyotarajiwa wiki jana tayari imeahirishwa mara mbili. Wakati huu, mmoja wa mawakili wa utetezi anabaini kwamba waziri wa zamani wa sheria anatarajia kuarifiwa hukumu yake leo Jumanne Septema 2. Kama ilivyo kwa kila kesi katika kesi hii, vikosi vya usalama vitatumwa karibu na Mahakama ya ya Juu ambapo majaji wanatarajiwa kutoa uamuzi wao.
Huu ni mwisho wa sakata ya kisheria iliyoanza majira ya kuchipua mwaka jana wakati Mwanasheria Mkuu alipowasilisha mbele ya mahakama shutuma zake za kwanza dhidi ya waziri huyo wa zamani kuhusu kandarasi ya ujenzi wa gereza jipya mjini Kisangani. Mwishoni mwa mwezi Mei, Constant Mutamba aliona mashtaka dhidi yake yakiidhinishwa na Bunge, na kesi yake ilianza Julai 9.
Utetezi wake umedumisha kutokuwa na hatia mara kwa mara. Mawakili wake wengi walijaribu kudhihirisha katika muda wote wa kusikilizwa kwa kesi yake kwamba mamlaka ilikuwa imefahamishwa kuhusu kesi hii na kuhusu kandarasi iliyopewa kampuni ya Zion Construction, kuonyesha nia njema ya mteja wao. Constant Mutamba anakabiliwa na kifungo cha miaka kumi gerezani na kupigwa marufuku ya miaka 20 kushikilia wadhifa wowote rasmi.