Mchakato wa amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umekwama. Wakati wajumbe bado wako Doha kwa karibu wiki mbili, lakini kwenye uwaja wa vita, mkwamo unasalia kati ya mapigano ya mara kwa mara na hatua ngumu kutekeleza za kujenga imani. Baada ya hotuba ya Félix Tshisekedi siku ya Jumamosi, Agosti 30, Corneille Nangaa amezungumza siku ya Jumatatu, Septemba 1, mjini Goma. Mvutano unaendelea kuongezeka kati ya kambi hizo mbili.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwenye uwanja wa vita, mapigano yameanza tena kwa nguvu katika maeneo kadhaa: katika mkoa wa Kivu Kusini, katika nyanda za juu za Uvira, Fizi, na Mwenga, lakini pia katika mkoa wa Kivu Kaskazini, haswa katika eneo la Walikale.

AFC/M23 inaishutumu Kinshasa kwa kushambulia ngome zake.

Kwa upande wake, Jeshi la DRC (FARDC) linashutumu vuguvugu la waasi, kwa mfano, kuchoma moto nyumba kadhaa mnamo Agosti 28 katika eneo la Ruberiki, huko Masisi. Pia linaishutumu kwa kuwakamata na kuwaweka kizuizini kinyume cha sheria vijana kadhaa, wakiwemo watoto wadogo, ambao walitumiwa “wakati mwingine kama wafuatiliaji, wakati mwingine kama ngao za binadamu,” pia huko Walikale, katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kwa wakati huu, hakuna upande ambao ambao umesusia au kujiondoa katika mazungumzo ya mchakato wa Doha, lakini kulingana na mratibu wa Muungano wa Mto Kongo (AFC), Corneille Nangaa, Rais wa Kongo Félix Tshisekedi-aliyejiimarisha kwa wanajeshi na vifaa-badala yake anatafuta kujionyesha kuwa ana nguvu. Anatishia: “Ichukulieni, kutakuwa na jibu linalofaa, hadi tishio litakapoondolewa kwenye chanzo chake.”

Siku mbili mapema, Félix Tshisekedi pia alitoa matamshi yenye utata. Wakati akikaribisha mchakato wa Doha na Washington, aliwakemea “Wakongo hawa wanaojiweka katika malipo ya majirani zao ambao tutapaswa kuwapiga hadi dakika ya mwisho,” kabla ya kuongeza: “Mazungumzo ndiyo, lakini na wale wanaotaka kujenga nchi na sio wale wanaotii amri za nchi jirani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *