Maofisa wawili wa juu katika jeshi la Congo ambao waliuawa katika shambulio la waasi wa M23, hapo jana walipewa heshima ya mazishi ya kitaifa jijini Kinshasa, wakati huu hali ya usalama mashariki mwa nchi hiyo ikisalia kuwa tete.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Luteni Jenerali Peter Cirimwami Nkuba, ambaye pia alikuwa gavana wa muda jimboni Kivu Kaskazini, pamoja na Brigedia Jenerali Alexis Rugabisha, walitunukiwa tuzo ya juu ya mashujaa wa nchi inayofahamika kama Kabila-Lumumba, katika sherehe zilizohudhuriwa na rais Felix Tschisekedi.

Cirimwami alifariki mwezi Januari mwaka huu baada ya kupigwa risasi jirani na mji wa Goma wakati akiratibu operesheni za kijeshi kuwazuia waasi wa M23 kuingia kwenye mji huo.

Maofisa wawili wa juu katika jeshi la Congo ambao waliuawa katika shambulio la waasi wa M23, hapo jana walipewa heshima ya mazishi ya kitaifa jijini Kinshasa.
Maofisa wawili wa juu katika jeshi la Congo ambao waliuawa katika shambulio la waasi wa M23, hapo jana walipewa heshima ya mazishi ya kitaifa jijini Kinshasa. © rdc

Jenerali Rugabisha, ambaye alikuwa akiongoza kikosi cha 12 cha uingiliaji kati wa haraka, nae aliuawa katika uwanja wa vita mwaka huu.

Mazishi haya yamefanyika wakati huu muungano wa Congo River, unaohusisha waasi wa M23, wakiituhumu serikali ya Kinshasa kukiuka makubaliano ya usitishaji mapigano.

Kiongozi wa muungano huo, Corneille Nangaa, sasa anaitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza shinikizo kwa utawala wa Kinshasa kuheshimu makubaliano waliyotiliana saini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *