Ulimwengu wote huungana kila Agosti 30 kuadhimisha siku ya kimataifa ya watu waliopotea.Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC inasema watu karibu laki tatu wameorodhesha kutoweka kote ulimwenguni,na wengine huenda wasiwahi kuunganishwa tena na familia zao.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika mpango maalum ICRC kwa ushirikiano na mashirika ya msalaba mwekundu katika mataifa mbali mbali,hujaribu kuwaunganisha wakimbizi waliotenganishwa kwa sababu ya vita au mizozo.
Nchini Kenya ICRC itatekeleza mpango huu kwa kushirikiana na shirika la msalaba mwekundu nchinini,katika kambi ya Daadab kaskazini mashariki na Kakuma,kaskazini mwa Kenya.

Faustina ,si jina lake halisi ni miongoni mwa wakimbizi kutoka kambi ya Kakuma ambaye amebahatika kurejesha mawasiliano na familia yake baada ya miaka karibu 20.

ICRC huwasaidia wakimbiza kuandika ujumbe kwa karatasi maalum ambao ICRC huwasilisha kwa shirika la msalaba mwekundu linalofanya kazi katika nchi anakotokea mkimbizi ili kufikisha kwa familia husika.
Ujumbe huo ukijibiwa,mkimbizi anaweza kuandika tena na kuomba namba ya simu kwa ajili ya mawasiliano na ikifanikiwa,anawezeshwa kupiga simu ya kawaida mara moja kwa mwezi au anaweza kupiga simu ya video kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp au Facebook,kutumia mtandao wa WIFI ambayo hugharamikiwa na ICRC na kuwekwa kwenye ofisi za msalaba mwekundu au maoneo maalum katika kambi.

Faustina aliandika ujumbe huo mara ya kwanza na japo ilichukua muda kujibiwa,majibu yalirudi na kumpa ari ya kuendelea kuandika.
Na mara ya pili,ujumbe wake uliporudi,uliambatana na namba ya simu ambayo anatumia hadi sasa kuzungumza na ndugu zake.
ICRC inasema ingawaje wakati mwingi,mpango huo huwa na changamoto,furaha yao kubwa ni kuona imerejesha tabasamu kwa hata familia moja.