
Takriban wanajeshi 2,000 wa Korea Kaskazini wameuawa katika mzozo wa kijeshi kati ya Urusi na Ukraine, mbunge wa Korea Kusini amesema Jumanne, Septemba 2, akinukuu takwimu za idara ya ujasusi ya nchi yake.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mwezi Aprili mwaka huu, “walikadiria idadi ya vifo kuwa angalau 600,” lakini kulingana na tathmini zilizosasishwa, “sasa wanakadiria idadi hiyo kuwa karibu wanajeshi 2,000,” Lee Seong-kweun amewaambia waandishi wa habari baada ya mkutano na idaar ya ujasusi ya Korea Kusini (NIS).
Idara ya ujasusi ya Korea Kusini na nchi za Magharibi zimedai kuwa Pyongyang imetuma zaidi ya wanajeshi 10,000 katika eneo la Kursk la Urusi mwaka 2024 wakati wa mashambulizi katika mji wa Kyiv, pamoja na makombora ya mizinga, makombora na mifumo ya roketi ya masafa marefu. Mbunge wa upinzani Lee Seong-kweun, mwanachama wa chama cha People Power Party cha rais wa zamani Yoon Suk Yeol, pia amedai kuwa taarifa za kijasusi za Korea Kusini zinakadiria kuwa Korea Kaskazini inapanga kupeleka wanajeshi wapya 6,000 nchini Urusi, 1,000 ambao tayari wamewasili.
Pyongyang na Moscow zimehusishwa na mikataba ya usalama na ulinzi tangu mwaka 2024
Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA liliripoti Jumamosi kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alizungumza siku moja kabla na familia za wanajeshi waliouawa katika mapigano dhidi ya Ukraine kuunga mkono Urusi. Tayari alikuwa amekutana na baadhi yao wiki iliyotangulia, wakati wa sherehe nyingine ya hadhara ya kwa niaba ya kuwakumbuka wanajeshi hao.
Pyongyang na Moscow zimehusishwa na makubaliano ya usalama na ulinzi tangu 2024. Kiongozi wa Korea Kaskazini atahudhuria gwaride kubwa la kijeshi huko Beijing siku ya Jumatano kuadhimisha miaka 80 ya kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia, ambapo viongozi wengine 25 wa kigeni, akiwemo Vladimir Putin, wanatarajiwa.
Moscow na Kyiv hazifichui jumla ya idadi ya wanajeshi waliotumwa katika mzozo huo. Mnamo mwezi Juni 2024, Rais wa Urusi Vladimir Putin alizungumza juu ya wanajeshi “karibu 700,000” wanaopigana nchini Ukraine, takwimu pia iliyotajwa mnamo mwezi Juni 2025 na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.