Chanzo cha picha, Getty Images
Ndege aina ya Boeing B-29 ilikuwa mshambuliaji mahiri zaidi wa Vita vya Pili vya Dunia, na ilikuwa ghali zaidi kuiunda kuliko mabomu ya nyuklia iliyodondosha. Pia ilisaidia kushawishi ujenzi wa ndege za kubeba abiria zinazotumika hii leo.
Ilikuwa miaka miwili kabla ya shambulio la Japan kwenye Bandari ya Pearl kuiingiza Marekani kwenye vita. Lakini Jeshi la Anga la Marekani lilikuwa linatafuta ndege mpya kutumika katika mashambulizi.
Kilichofuata ni uundaji wa ndege aina ya “superbomber”, yenye uwezo wa kuruka hadi maili 2,000 (3,200km) kwa wakati mmoja na kwenye miinuko ambayo haikuwahi kufikiwa hapo awali.
Ndege waliyopata ilitupa mabomu ya atomiki huko Hiroshima na Nagasaki na hatimaye kukomesha Vita vya Pili vya Dunia.
Pia ilifungua njia ya kuimarika kwa usafiri wa anga ambao unaotumika na ndege za abiria kila siku.
Hii ni hadithi ya jinsi ndege iliyogharimu zaidi ya mradi mzima wa Manhattan – B-29 Superfortress – ilivyobadilisha ulimwengu.
Ilikuwa Januari 1940 wakati Jeshi la Anga la Marekani (USAAC) lilipoziomba kampuni tano za ndege za Marekani kujenga bomu kubwa kuliko kitu chochote ambacho ulimwengu umewahi kuona.
Ingawa Marekani ilikuwa bado haijaingia kwenye Vita vya pili vya dunia, huko Ulaya ilikuwa tayari vita vimepamba moto: Ujerumani ya Nazi na Umoja wa Kisovieti miezi kadhaa mapema ziliivamia Poland na kuigawanya kati yao. Marekani ilijua ni suala la muda tu kabla ya kuingia katika mgogoro huo.
Ndege ambayo Marekani iliitaka ingelazimika kuruka zaidi na juu zaidi kuliko ndege yoyote ambayo ilikuwa imetengenezwa. Hiyo iligeuka kuwa changamoto kubwa, hata kwa taifa kubwa lenye viwanda duniani.
Kati ya kampuni mbili zilizoombwa kutengeneza ndege hiyo, Douglas na Lockheed, zililazimika kuwacha baadhi ya kazi zilizokuwa nazo. Boeing, hata hivyo, ilikuwa kifua mbele , baada ya kuanza kazi ya kubuni mradi kama huo wa kibinafsi miaka michache mapema.
Ndege iliovuruga bajeti ya Marekani
Muundo wa Boeing XB-29 hatimaye ulishinda shindano la USAAC, lakini ilichukua miaka mingine minne kabla ya ndege hiyo iliyojulikana kama B-29 Superfortress kuanza kuhudumu.
Ulikuwa mradi ghali na mgumu zaidi wa kiviwanda ambao tasnia ya Marekani iliwahi kuufanya na haungepita hadi mipango ya anga katika miaka ya 1950 na 1960. Na ilisukuma teknolojia ya anga kupita kikomo chake.
Chanzo cha picha, Getty Images
Mradi wa B-29 ulikuwa ghali zaidi katika vita vyote – ukigharimu karibu 50% zaidi ya Mradi wa Manhattan uliounda mabomu ya kwanza ya atomiki duniani.
Katika pesa za leo ndege hiyo, kuanzia muundo hadi kukamilika, ingegharimu sawa na $55.6bn (£41.2bn).
Ndege hizo ambazo ziliundwa miaka michache ya kwanza ya Vita vya dunia vya pili zilikuwa na mpango wa kutekeleza misheni yao zaidi ya 20,000ft (6km).
Kadiri unavyoruka juu, ndivyo unavyoweza kuruka kwa muda mrefu, kwa sababu hewa sio nzito, lakini ilisababisha changomoto chungu nzima kwa maafisa waliokuwa ndani yake.
Kasi ya juu ya kushambulia ndege katika Vita vya Pili vya Dunia ilimaanisha kuwa ndege za kivita zilikuwa na sekunde moja tu ya kuchagua shabaha
Boeing ilibadilika na kuwa na mpango mpya unaoleta tumaini . Hii ilimaanisha kuwa chumba cha ndege kilikuwa na shinikizo la hewa sawa na maudhui ya oksijeni ambayo ungepata ardhini – ambayo ilimaanisha kuwa wafanyakazi hawakuhitaji kuruka na vifaa vya oksijeni.
Hewa ingevutwa nje ya injini, kupozwa, kusafishwa na kisha kusukuma ndani ya vyumba vya walenga shabaha. Inaweza pia kupashwa joto ili wahudumu wasilazimike kuvaa nguo nzito kujikinga na baridi.
Teknolojia hiyo ilikuwa ikifanyiwa utafiti tangu miaka ya 1920, lakini lengo likiwa majaribio. B-29 ilikuwa ndege ya kwanza ya kivita kuzalishwa kwa wingi .
“Iliruhusu wahudumu kufanya kazi wakiwa wamevalia suti nyepesi za ndege, kwa sababu vyumba vyake vilikuwa vimepashwa joto, hali iliowafanya kutekeleza misheni za muda mrefu zaidi katika mazingira bora zaidi,” anasema Jeremy Kinney, mfanyakazi katika Jumba la Makumbusho ya Kitaifa ya Anga Smithsonian huko Washington DC.
Chanzo cha picha, Getty Images
Kuijaza oksijeni ndege yote ilikuwa ngumu na ghali. Badala yake, Boeing ilibuni vyumba vitatu tofauti vyenye hewa kwa wahudumu 11 wa B-29. Sehemu ya kwanza kwenye pua ya ndege ilikuwa na rubani, rubani mwenza, mshambuliaji, mwelekezi, mwendeshaji wa redio na mhandisi wa ndege – wa mwisho akiwa na jukumu la kufuatilia injini nne kubwa na zenye joto za ndege.
Kati ya sehemu ya kwanza na ya pili ya wahudumu – kipande cha kwanza cha ndege kilikuwa kimebeba bomu kubwa na juu yake – kulikuwa na handaki ambalo wahudumu wangeweza kutambaa. Chumba cha kati, ambapo walenga shabaha na mwendeshaji rada walihudumu, kilikuwa na choo cha kemikali na baadhi ya vyumba vya kulala.
“Kulikuwa na hatari fulani,” anaonya Hearn. “Ikiwa ulikuwa na ukosefu wa ghafla wa hewa kwenye handaki linalotumika kusonga kati ya vyumba tofauti, unaweza kupigwa risasi haraka sana, hali iliokuwa ya kutatanisha na inayotia wasiwasi.”
Bunduki zinazotumia rimoti
Kasi ya juu ya kushambulia ndege katika Vita vya Pili vya Dunia ilimaanisha kwamba ndege hizo za kivita zilikuwa na sekunde moja pekee kuchagua shabaha.
Mnamo 1944, ndege za kivita zilikuwa zikiongezeka kwa kasi . Sehemu zenye shinikizo za B-29 ziliruhusu wabunifu wafikirie zaidi, na wakaja na mpango mpya: bunduki zinazodhibitiwa kwa mbali.
Walenga shabaha hawakulazimika kuelekeza bunduki wenyewe, wakitarajia kubahatika wakati ndege hizo zilishambulia umbali mrefu wa maili moja kwa saa.
Badala yake, mfumo mpya wa kudhibiti risasi ulikokotoa lengo la washambuliaji hao kwa kutumia rada ambayo inaweza kusoma halijoto ya hewa na kumimina risasi. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa ndege kuwa na uwezo kama huo.