Chanzo cha picha, Getty Images
Aston Villa hawakupokea ofa kutoka Manchester United kwa ajili ya kipa wa Argentina Emiliano Martinez licha ya mchezaji huyo mwenye miaka 32 kuhusishwa sana na uhamisho wa kuelekea Old Trafford. (Sky Sports)
Manchester United waliamua kutomchukua Martinez kwa sababu ya umri wake na mshahara unaokaribia pauni 200,000 kwa wiki. (Mirror)
Martinez hakuwa na hamu ya kujiunga na Galatasaray licha ya ripoti kutoka Uturuki kuhusu ofa ya thamani ya pauni milioni 21.6. (Daily Mail)
Liverpool walikataa kumruhusu Joe Gomez, 28, kujiunga na AC Milan baada ya mpango wao wa kumsajili beki wa England Marc Guehi, 25, kutoka Crystal Palace kuvunjika. (Fabrizio Romano)
Video ya kuaga ya Guehi kutoka Crystal Palace ilivuja mitandaoni lakini bado ameridhika kumalizia mwaka mmoja wa mkataba wake Selhurst Park na kisha kuondoka bure msimu ujao wa kiangazi. (Talksport)
Chanzo cha picha, Getty Images
Bayern Munich walitaka kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman, 27, kutoka Atalanta kwa mkopo siku ya mwisho ya dirisha la usajili. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Kiingereza wa Chelsea Raheem Sterling anaonekana kubaki Stamford Bridge kwani hakuna timu kutoka Uturuki, Saudi Arabia au Marekani zilizoonyesha nia ya kumsajili nyota huyo mwenye miaka 30 hata kama madirisha yao ya usajili bado yako wazi. (The Athletic)
Crystal Palace walijiondoa katika mpango wa mkopo wa mshambuliaji wa Tottenham, Manor Solomon, 26, kutoka Israeli licha ya kuwepo kibali kilichowaongezea muda wa kukamilisha usajili huo. (Sky Sports)
Chanzo cha picha, Getty Images
Uhamisho wa kiungo wa Wales Harry Wilson kutoka Fulham kwenda Leeds ulivunjika baada ya Fulham kubadili uamuzi dakika za mwisho kuhusu kumuuza mchezaji huyo mwenye miaka 28. (Yorkshire Evening Post)
Kuvunjika kwa uhamisho wa Wilson pia kulihitimisha uwezekano wa Chelsea kumpeleka Fulham kwa mkopo winga wa Kiingereza Tyrique George mwenye miaka 19. (Evening Standard)
Mshambuliaji wa Denmark Will Osula, 22, atabaki Newcastle United licha ya kuvutiwa na Eintracht Frankfurt waliotaka kumsajili kwa mkopo wa msimu mzima siku ya mwisho ya dirisha la usajili. (Athletic)
Vyanzo vya ndani vya Newcastle United vimesema mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 25, alikuwa akicheza na kuonyesha tabia kana kwamba hataki timu hiyo ifuzu Ligi ya Mabingwa kuanzia mwezi Aprili. (Telegraph)