[ad_1]

a

Chanzo cha picha, Israel Foreign Ministry X

Maelezo ya picha, Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Israel, satelaiti ya kijasusi ya “Horizon 19” ilirushwa angani kutoka kituo cha anga cha Belmahim katikati mwa Israel.

Israel imesema imefanikiwa kurusha satelaiti mpya ya kijasusi angani, hatua ambayo itaimarisha kwa kiwango kikubwa uwezo wake wa upelelezi katika eneno la Mashariki ya Kati. Kwa mujibu wa maafisa wa Israel, satelaiti hii inaweza kupiga picha za vitu vidogo hadi ukubwa wa sentimita 50, mchana na usiku.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, alisema uzinduzi wa satelaiti hiyo, iliyopewa jina la “Horizon 19,” ni ujumbe wa moja kwa moja kwa maadui kwamba “tunawaangalia kila wakati na katika hali zote.”

Bw. Katz alielezea urushaji huo kuwa ni “mafanikio ya hali ya juu kabisa” ambayo ni mataifa machache pekee duniani yanaweza kuyafikia.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Israel, satelaiti hiyo ilirushwa angani usiku wa Jumanne, Septemba 2, kwa msaada wa roketi cha Shavit, na kufika kwenye obiti ya dunia kwa mafanikio.

[ad_2]

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *