.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Makka, Kaaba na Msikiti Mkuu. Picha ilichapishwa Paris mnamo 1790.

Ingawa leo hii ardhi ya Hijaz haina kabisa wafuasi wa Uyahudi na Ukristo au dini nyingine yoyote isipokuwa Uislamu, isipokuwa kwa baadhi ya wageni au wafanyakazi wa kigeni, wanahistoria wengi wanaamini kwamba dini hizi mbili zina historia ya kale sana huko Makka na Madina, miji miwili mitakatifu ya Uislamu.

Kulingana na wanahistoria hawa, Waarabu walifahamu Dini ya Kiyahudi huko Bethlehemu angalau karne tano kabla ya Kristo, ingawa kuna kutokubaliana kuhusu wakati hasa ambao dini hii iliingia katika nchi ya Waarabu.

Vitabu vya Agano la Kale vya Mambo ya Nyakati katika Biblia vinaeleza kwamba makabila ya Wasimeoni yalihama kutoka Mlima Sinai na mifugo yao ili kutafuta malisho na kufika eneo la makabila ya Maan (kusini mwa Yordani ya sasa).

Huko, vita vikali vilifanyika ambavyo viliisha kwa ushindi wa Wasimeoni.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *