Modi, Putin na Xi wakiwa wamesimama ana kwa ana wakiwa wamevalia suti nyeusi au fulana

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kabla ya Tianjin, viongozi hao watatu walikutana hapo awali Kazan mwaka jana

    • Author, Osmond Chia
    • Nafasi, Mwandishi masuala ya biashara, BBC News

Mkutano wa Jumatatu wiki hii kati ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, Rais wa China Xi Jinping, na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi uliashiria mshikamano wa nadra –na ulikuwa fursa mahsusi kwa Putin kuwasiliana moja kwa moja na wanunuzi wakubwa wa mafuta ya Urusi.

India na China zilivutiwa na mafuta ya Urusi baada ya bei kushuka wakati mataifa ya Magharibi kukata mahusiano ya kibiashara na Moscow kufuatia uvamizi wa Ukraine mwaka 2022.

Hata hivyo, uhusiano kati ya Beijing, New Delhi na Moscow sasa umejikita zaidi ya biashara ya mafuta.

Mataifa haya matatu sasa yanakutana kwenye msingi wa msimamo wa pamoja dhidi ya Marekani ambayo imeiwekea Urusi vikwazo vikubwa vya kiuchumi na kutoza ushuru mkubwa kwa washirika wake wa kibiashara.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *