a

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lissu

Hatma ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, inatarajiwa kujulikana leo Jumatatu, Septemba 15, 2025, wakati Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, itatoa uamuzi wa hatimaye kuamua kama kesi ya uhaini inayomkabili mshtakiwa (Case No. 19605/2025) itafutwa, itarudishwa Kisutu au kuendelea Mahakama Kuu.

Uamuzi huu unatarajiwa kutolewa na jopo la majaji watatu (3), likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, huku majaji wengine wakiwa James Karayemana na Ferdinand. Jopo hili ndilo limepitisha masuala yote ya mapingamizi yaliyowasilishwa na Lissu.

Tundu Lissu amewasilisha mapingamizi mawili. Pingamizi la kwanza, ambalo tayari limesikilizwa, linahusu mamlaka ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusikiliza kesi yake, huku Lissu akidai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haikuwa na mamlaka ya kisheria kuendesha mchakato wa awali. Pingamizi la pili litasikilizwa baada ya Mahakama kutoa uamuzi juu ya pingamizi la kwanza; linalenga hoja yake kwamba Hati ya Mashitaka iliyotolewa Kisutu ni mbovu kisheria, haiwezi kuendelea bila marekebisho.

Katika hoja zake, Lissu ameibua hoja tano kuu:



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *