
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema vitisho kutoka kwa maadui wa Jamhuri ya Kiislamu vinaendelea tangu kujiri mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya nchi hii.
Mohammad Eslami ambaye anaongoza Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) ameeleza haya kwa shirika la habari la Japan la Kyodo katika mahojiano ya maandishi yaliyochapishwa jana Jumatano.
Eslami amesema kuwa hali ya mambo ya sasa inasalia kuwa sawa na ya wakati wa vita kutokana na uwepo wa hatari ya Israel kutekeleza mashambulizi mapya.
Utawala wa Israel mwezi Juni mwaka huu ulianzisha vita vya kichokozi dhidi ya Iran na kutekeleza mashambulizi makubwa na ya uharibifu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliyozilenga taasisi za nyuklia, miundombinu ya ulinzi, maafisa wa kijeshi, wanasayansi wa nyuklia, na raia wa kawaida. Watu wasiopungua 935 wakiwemo watoto wadogo waliuliwa shahidi katika mashambulizi hayo yaliyodumu kwa siku 12.
Marekani ilijiunga na vita vya Israel wakati hujuma hiyo ikiendelea na kushambulia vituo kadhaa vya nyuklia muhimu vya Iran.
Kama alivyobainisha Eslami, “”Hii ni mara ya kwanza katika historia kuona taasisi za nyuklia zilizokuwa zikilindwa zimekabiliwa na mashambulizi ya kijeshi.