
Idadi ya vifo vya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza inaendelea kuongezeka huku mashambulizi ya kijeshi na mauaji ya kimbari ya Israel yakiingia mwaka wa pili sasa, na hivyo kuzidisha ukosoaji kimataifa.
Miito mbalimbali imetolewa kuiwekea vikwazo Israel na kuutenga utawala huo kutokana na mauaji ya kimbari kutokana na mauaji ya kimbari inayoendelea kufanya dhidi ya wakazi wa Gaza.
Wizara ya Afya ya Gaza jana iliripoti kuwa watu 98 wameuawa shahidi na 385 kujeruhiwa katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita.
Tangu kuanza vita na mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Gaza Oktoba 7, mwaka 2023 Wapalestina wasiopungua 65,062 wameuawa shahidi na wengine 165,697 kujeruhiwa katika eneo hilo.
Wizara ya Afya ya Gaza pia imeripoti kuwa watu 432 wakiwemo watoto 146 wamepoteza maisha kutokana na njaa na utapiamlo tangu kutangazwa baa la njaa katika ukanda huo unaokabiliwa na mzingiro.
Maafisa wa afya wametahadharisha kuhusu kusambaratika mfumo wa matibabu wa Gaza, wakitaja kuendelea kuzuiwa kwa mafuta hatua iliyoathiri huduma za hospitali.
Wizara ya Afya ya Gaza imeituhumu Israel kwa kuzuia kwa makusudi juhudi za Shirika la Afya Duniani kusambambaza mafuta huko Gaza.