Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kigezo “kilichofanikiwa” cha ushirikiano kati ya nchi huru, zikiwemo na Iran na Russia, utathibitisha kwamba zama za uchukuaji hatua za upande mmoja duniani zimemalizika.

Rais Pezeshkian ameyasema hayo katika mazungumzo na Waziri wa Nishati wa Russia Sergei Tsivilev na ujumbe alioandamana nao na kubainisha: “tutaweza kuziongoza nchi zetu kwenye maendeleo na upigaji hatua bila ya kuhitaji au kutegemea madola yanayojichukulia hatua za upande mmoja”. 

Ameongeza kuwa, Iran na Russia zimeazimia kutekeleza makubaliano yaliyotiwa saini hapo awali kati ya nchi mbili katika nyanja za usafirishaji, nishati na mitambo ya kuzalisha umeme, na kuwataka wataalamu na mawaziri wa pande zote mbili kufanya juhudi maradufu katika kufanikisha suala hilo.

Rais wa Iran amesema: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafuatilia kwa dhati utekelezaji wa makubaliano kati ya nchi mbili … hakuna kikwazo katika njia ya ushirikiano wa Tehran na Moscow na kutekelezwa makubaliano baina ya pande mbili”.

Dk Pezeshkian ameeleza kwamba anatumai mabadilishano ya ziara kati ya maafisa wa kidiplomasia wa Iran na Russia yatapelekea kukuza zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili “rafiki na washirika”.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati wa Russia Sergei Tsivilev, amewasilisha salamu za Rais Vladimir Putin wa Russia kwa Rais wa Iran na kueleza kuridhishwa na ushirikiano wenye kujenga wa pande mbili kupitia mfumo wa Tume ya Pamoja ya Kiuchumi ya Iran na Russia.

Aidha, ameelezea utayarifu wa Russia wa kutekeleza bila kuchelewa makubaliano iliyofikia na Iran, akisisitiza kwamba hakuna vikwazo au mashinikizo ya nje yanayoweza kukwamisha ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya nchi mbili.

Iran na Russia zikiwa washirika wawili wa karibu na wa kistratejia, zimestawisha uhusiano wao katika nyuga mbalimbali licha ya kuwekewa vikwazo vikali na nchi za Magharibi…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *