Laurent Gbagbo Rais wa zamani wa Ivory Coast amesema hatomuunga mkono mgombea yeyote katika uchaguzi ujao wa rais.

Licha ya kutangazwa kuwa hana sifa za kugombea katika uchaguzi ujao huko Ivory Coast, Gbagbo ametangaza kuwa hatomuunga mkono yeyote kati ya wagombea waliopitishwa na Baraza la Katiba.

Msemaji wake, Me Habiba Toure amesema kuwa kushindwa kufikiwa mapatano na baadhi ya wagombea kutostahiki kuwania kiti cha urais ndio saabu iliyompelekea Laurent Gbagbo kuchukua uamuzi huo. 

Msemaji wa Laurent Gbagbo amesisitiza kuwa wagombea walioidhinishwa na Baraza la Katiba la Ivory Coast hawawakilishi vyama vikubwa vya kisiasa nchini humo.

Simone Gbagbo mke wa zamani wa Laurent Gbagbo ni kati ya wagombea wakuu wa kiti cha urais katika uchaguzi ujao wa Rais wa Ivory Coast.

Gbagbo ambaye mara kwa mara amekuwa akipinga azma ya Rais wa sasa Alassane Ouattara kuwania muhula wa nne wa urais, ameitaja hatua hii kuwa ni ukiukaji wa sheria na katiba.

Naye Msemaji wa serikali, Amadou Coulibaly ametahadharisha kuwa changamoto zozote katika maamuzi ya Baraza la Katiba zitakuwa na taathira za kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *