Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ameipongeza kwa dhati timu ya mieleka ya mtindo wa Greco-Roman ya Iran kwa kutwaa taji la ubingwa wa dunia katika Mashindano ya Dunia ya Mieleka ya mwaka 2025 yaliyofanyika nchini Kroatia.

Katika ujumbe wake wa Jumapili, Ayatullah Khamenei amepongeza “azma na juhudi za dhati” za wanamasumbwi hao, akisema wameliletea furaha na fahari taifa zima.

Amesema: “Hongereni vijana wanamieleka. Azma na juhudi zenu pamoja na za ndugu zenu wa masumbwi ya mtindo wa freestyle zimeifurahisha taifa na kuipa heshima nchi yetu. Namuomba Mwenyezi Mungu awajaalie mafanikio na ushindi zaidi. Nawapongeza wanamichezo, makocha na wasimamizi wote.”

Timu hiyo ya Iran ya Greco-Roman ilitwaa ubingwa wa Mashindano ya Dunia yaliyofanyika mjini Zagreb, siku moja kabla ya mashindano hayo kufikia tamati. Iran ilikusanya medali nne za dhahabu, mbili za fedha na mbili za shaba, na kufikisha jumla ya pointi 180—ikizishinda Jamhuri ya Azerbaijan (89) na Uzbekistan (72).

Ushindi huu ulifuata kwa karibu mafanikio ya kihistoria ya timu ya freestyle ya Iran, ambayo ilitwaa ubingwa wa dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12, kwa medali saba za kihistoria.

Timu ya freestyle ya Iran iliongoza kwa pointi 145, ikifuatiwa na Marekani (134) na Japan (111).

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya mieleka ya Iran kwa timu zote mbili—freestyle na Greco-Roman—kutwaa ubingwa wa dunia katika mwaka mmoja. Hakika, ni mwaka wa neema kwa masumbwi ya Iran.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *