
Wananchi wa Tunisia wamefanya maandamano katika mikoa na miji mikubwa yote ya nchi hiyo kuunga mkono kundi la Global Fleet of Resistance na pia kuunga mkono mapambano ya kuhakikisha vita vinakomeshwa Ghaza na mzingiro wa kidhulma dhidi ya ukanda huo unavunjwa.
Mwandishi wa Televisheni ya Al-Alam nchini Tunisia ameripoti kwa kusema: “Watunisia wamepaza sauti zao kwa kaulimbiu za kuunga mkono Ghaza na msafara wa meli za Global Fleet of Resistance zinazosafiri baharini kujaribu kuvunja mzingiro wa Ghaza.
Jawaher Shana, mjumbe wa kamati ya maandalizi ya Global Resistance Fleet, ameiambia televisheni ya Al-Alam kwamba: “Meli hizo kwa sasa zinakaribia eneo la Ugiriki baada ya meli zake 12 kushambuliwa na Israel usiku wa jana. Kuna vitisho vya kuripua meli usiku wa leo, na vitisho hivyo vinaweza kuwa vikali zaidi. Meli bado ziko salama kuelekea Ghaza.”
Kwa mujibu wa Al-Alam, mashirika mbalimbali yakiwemo ya Popular Movement, National Democratic Party na Muungano Mkuu wa Wafanyakazi wa Tunisia yameshiriki katika maandamano hayo na mikutano ya hadhara, lengo likiwa ni kuunga mkono msafara wa meli za kupambana na Wazayuni ili waache kuuzingira Ukanda wa Ghaza.
Samir Cheffi, naibu katibu mkuu wa Umoja wa Wafanyakazi wa Tunisia, pia ameiambia televisheni ya Al-Alam kwamba: “Hili ni jaribio la kukata tamaa na lisilo na matumaini linalofanywa na Wazayuni kujaribu kuwatisha vijana; lakini tunautangazia (utawala wa Kizayuni) kwamba meli hizi, ambazo sasa zimefikia makumi ya boti na meli, ni wimbi la mamilioni ya watu, hazizuiliki.”