Urusi na China zimeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuipigia kura rasimu ya azimio la kuchelewesha kwa miezi sita vikwazo dhidi ya Iran.

Vikwanzo vyote vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran vinatazamiwa kuanzishwa tena leo Ijumaa usiku baada ya Ufaransa, Uingereza na Ujerumani kuchochea mchakato wa siku 30, zikiituhumu Tehran kwa kukiuka mkataba wa 2015 na mataifa hayo yenye nguvu kiuchumi duniani, juu ya shughuli zake za nyuklia.

Iran na mataifa hayo matatu ya Ulaya, mnamo wiki hii yamekuwa yakijaribu kufikia makubaliano ya mwisho ili kuchelewesha kurejeshwa kwa vikwazo na kutoa nafasi kwa mazungumzo ya muda mrefu kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.

Wanadiplomasia walisema matarajio ya kuepusha vikwazo bila makubaliano kati ya Iran na nchi hizo ni finyu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *