Wakati huu kikao cha umoja wa Mataifa kikiendelea jijini New York, Marekani, nyuma ya pazia juhudi za kumaliza vita ya Sudan zimeshika kasi, wakati huu mzozo wa nchi hiyo ukisababisha mamilioni ya watu kuwa wakimbizi na wengine maelfu kuuawa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wanadiplomasia wanaohusika katika mchakato huo akiwemo Alan Boswell kutoka shirika la kimataifa la utatuzi wa mizozo kwenye kanda ya pembe ya Afrika, amesema mikutano inaendelea na kuna Imani kubwa kuwa muafaka utapatikana.

Kauli yake anaitoa wakati huu ambapo kwa mara ya kwanza tangu vita ya Sudan ianze miaka miwili iliyopita, mataifa yenye nguvu yalikubaliana kuhusu mpango utakaosaidia kuleta amani ya kudumu kwenye taifa hilo.

Hata hivyo wakati juhudi za upatanishi zikiendelea, jeshi limetangaza kutounga mkono mpango ulitolewa na nchi za Magharibi, likisema haliko tayari kushiriki mazungumzo na RSF inayowaita magaidi.

Kwa mujibu wa umoja wa Mataifa, watu Zaidi ya elfu 40 wameuawa na karibu milioni 13 hawana makazi na wanakabiliwa na baa la njaa huku milioni 24 wakiwa hawana chakula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *