
Jiji kuu la Madagascar, Antananarivo, limesalia mahame baada ya maandamano makubwa ya Alhamisi ya wiki hii yaliyoshuhudia vurugu, ambapo raia walijitokeza barabarani kupinga mgao wa umeme wa mara kwa mara pamoja na uhaba wa maji.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakazi waliopigwa na butwaa wengine wakitoa machozi walitathmini uharibifu huo Ijumaa asubuhi wakati ripoti za uporaji zikiendelea kuripotiwa nje kidogo ya mji mkuu, Antananarivo.
Maandamano ya siku ya Alhamisi, yaliyohusisha maelfu ya vijana, yalipata upinzani kutoka kwa polisi waliokuwa wakitumia risasi za mpira na mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya.
Ghasia ziliendelea hadi usiku na kulazimu polisi kutangaza makataa ya kutotembea usiku hadi saa kumi na moja asubuhi kuruhusu kurejea kwa utulivu baada ya benki na maduka kuporwa na hata kuteketezwa moto.
Baadhi ya watu wanaituhumu serikali ya rais Andry Rajoelina kwa kushindwa kuboresha hali ya maisha, katika kisiwa hicho kinachokabiliwa na hali ya umaskini.