Mkurugenzi wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani FBI na mkosoaji maarufu wa Donald Trump James Comey, amefunguliwa mashtaka kwa makosa mawili ya jinai wakati Rais Trump akizidisha kampeni ya hatua za kisheria dhidi ya maadui wake kisiasa.

Mashtaka hayo yamefunguliwa siku chache baada ya Trump kutamka hadharani akimtaka Mwanasheria Mkuu wa serikali Pam Bondi kuchukua hatua dhidi ya Comey na wengine anaowaona kuwa maadui.

Comey ameshtakiwa kwa kutoa taarifa za uongo na kuzuia haki kuhusiana na uchunguzi aliofanya kuhusu iwapo Urusi iliingilia uchaguzi wa 2016 ambao Trump alishinda na endapo Trump alishirikiana na Urusi.

Trump amepongeza mashtaka hayo, akisema Comey ni mmoja ya watu wabaya zaidi kuwahi kutokea Marekani. Iwapo atapatikana na hatia, Comey anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano jela.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *