Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa hatoruhusu mshirika wake wa karibu Israel kuunyakua Ukingo wa Magharibi, baada ya baadhi ya mawaziriwa nchi hiyo kutishia hatua hizo ili kuzima matumaini ya suluhisho la mataifa mawili.

Trump ametoa matamshi hayo baada ya kuulizwa iwapo aliwaahidi viongozi wa nchi za Kiarabu wakati wa mkutano katika Umoja wa Mataifa wiki hii kwamba angezuia unyakuzi wowote.

Alipoulizwa kama amemuonya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu dhidi ya suala hilo wakati wa mazungumzo yao hapo jana, Trump alikiri kwa kusema kwamba ndio amefanya hivyo lakini hatokubali Ukingo wa Magharibi kunyakuliwa.

Trump pia alielezea matumaini kuhusu makubaliano ya amani ya Gaza huku kukiwa na shinikizo linaloongezeka la kukomesha vita na kuachiliwa mateka wanaoshikiliwa na kundi la wanamgambo la Hamas.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *