Akizungumza na wanahabari jijini New York, Pezeshkian amesema suala hilo halikubaliki. Ametoa kauli hiyo wakati Umoja wa Mataifa ukitazamiwa kuiwekea tena vikwazo Iran Jumamosi baada ya mazungumzo na nchi za magharibi kuhusu mpango wake wa nyuklia kukwama.   

Iran yadaiwa kuongeza Urani iliyorutubishwa

Mwanzoni mwa mwezi Septemba, Shirika la Kudhibiti Nyuklia la Umoja wa Mataifa liliripoti kuwa asilimia 60 ya hifadhi ya Urani iliyorutubishwa na Iran ilifikia kilo 440 mwezi Juni ambazo ni ongezeko la kilo 32 tangu mwezi Mei.

Baadhi ya nchi za Ulaya zilianzisha mchakato wa kuirejeshea vikwazo Iran mwezi mmoja uliopita zikidai Iran imepuuza ahadi zake chini ya makubaliano ya nyuklia yanayoiwezesha kuondolewa vikwazo vya kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *