Kurejeshwa tena kwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran siku ya Jumamosi kuhusiana na mpango wake wa nyuklia sasa ni jambo lisiloepukika, kufuatia kukataliwa siku ya Ijumaa, Septemba 26, azimio la mwisho katika Baraza la Usalama ambalo lingewezesha kuahirishwa kuanza kutumika Jumamosi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Ijumaa Baraza hilo limetupilia mbali pendekezo la Urusi na China la kuongeza muda wa makubaliano ya 2015 ya kudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran kwa miezi sita ili kubadilishana na kuondolewa kwa vikwazo. Azimio la Urusi na China lilikataliwa na nchi 9 kati ya 15 wanachama.

Kwa hivyo, “vikwazo […] vitawekwa tena mwishoni mwa juma hili,” amesema Balozi wa Uingereza Barbara Woodward. “Kwa masikitiko yetu makubwa, Iran imeendelea kukataa. Tulitarajia ishara, lakini ishara halisi na maalum.” “Iran haijatoa ishara yoyote ambayo ni halisi na sahihi,” amelezea Jérôme Bonnafont, mwenzake wa Ufaransa.

Iran yashtumu kurejeshwa kwa vikwazo “batili kisheria”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametangaza urejeshwaji wa vikwazo wa Umoja wa Mataifa Jumamosi kuwa ni “batili kisheria.” “Msimamo wa Iran kuhusu E3” [Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, ] kuchochea mchakato wa kurejesha vikwazo “ni wazi na thabiti: ni batili kisheria, ni hatari kisiasa, na ina dosari za kiutaratibu,” Abbas Araghchi ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Iran “kamwe haitakubali shinikizo” juu ya mpango wake wa nyuklia. “Tunajibu kwa heshima tu. Chaguo liko wazi: ongezeko la mzozo au diplomasia,” Abbas Araghchi ameongeza kwa vyombo vya habari. Hata hvyo, Rais wa Iran Massoud Pezeshkian  amebainisha kuwa nchi yake haitajiondoa kwenye Mkataba wa Kuzuia Usambazaji wa Nyuklia (NPT). “Hatuna nia ya kuondoka NPT,” amewaambia waandishi wa habari kando ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, akionya mataifa ya kigeni dhidi ya kuunda “kisingizio cha juu cha kuchochea uhasama katika eneo hilo.”

Kuelekea juhudi za kidiplomasia zinazoendelea?

“Hii sio diplomasia, ni udanganyifu, uwongo, na ukumbi wa michezo wa kipuuzi,” amekashifu Naibu Balozi wa Urusi Dmitry Polyanskiy, akishtumu “unafiki” wa Ulaya mbele ya “hekima ya kimkakati na kubadilika kwa kidiplomasia.” Urusi imesema haitatekeleza vikwazo vya Umoja wa Mataifa. “Hakuna vikwazo na hakutakuwa na vikwazo.” “Jaribio lolote la kufufua maazimio ya yaliyopo ya Baraza la Usalama dhidi ya Iran kabla ya 2015 ni batili na hayana msingi,” amesema Naibu Balozi wa Urusi Dmitry Polyanskiy.

Mabalozi wa Uingereza na Ufaransa hata hivyo wamesisitiza kuwa kurejeshwa kwa vikwazo hakumaanishi mwisho wa juhudi za kidiplomasia. “Tuko tayari kuendelea na majadiliano na Iran kwa ajili ya suluhu la kidiplomasia ili kushughulikia masuala ya kimataifa kuhusu mpango wake wa nyuklia,” amesema Barbara Woodward. “Kwa kuanzishwa kwa mazungumzo hayo kunaweza kuruhusu kuondolewa kwa vikwazo katika siku zijazo,” ameongeza.

Jérôme Bonnafont amesisitiza kwamba vikwazo hivi vinapaswa kuonekana kama “kigezo” cha kufikia “makubaliano thabiti, ya kudumu na yanayoweza kuthibitishwa” ya kudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *