
Shehena kuu wa setilaiti ya Nahid-2 ya Iran, ambayo ilizinduliwa mwezi Agosti, kwa sasa inafanyiwa majaribio katika obiti. Shehena hiyo ina jukumu muhimu katika kuanzisha mawasiliano ya satelaiti.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Hassan Salarieh, Mkuu wa Taasisi ya Anga za Juu ya Iran, amesema kwenye mahojiano maalumu kwamba satelaiti ya mawasiliano ya “Nahid-2” kwamba: Satelaiti hii imerushwa na hivi sasa iko katika hatua ya majaribio ya kwenye obiti.
Ameendelea kusema: Mifumo midogo mingi imewashwa tayari na kwa sasa shehena yake muhimu zaidi yaani mfumo mdogo wa mawasiliano wa Q-band, nao unafanyhiwa majaribio. Mfumo huo unaruhusu mawasiliano ya kipimo data cha juu kuliko mawasiliano yote ya awali. Amesema: Majaribio mengi yameshafanywa kwenye hatua hii na zimebakia changamoto chache.
Hassan Salarieh, Mkuu wa Taasisi ya Anga za Juu ya Iran pia amesema: Kinachofanyika kwa sasa ni taratibu za udhibiti wa satelaiti na uimarishaji wake. Tayari taratibu za kuimasha mzunguko wa obiti umeshafanywa na sasa setilaiti inafanyiwa majaribio yanayohusiana na uwezo wake.
Akizungumzia maendeleo yaliyofikiwa kuhhusu mradi huo, mkuu huyo wa Shirika la Anga la Iran amesema: “Mchoro wa pili wa satelaiti umefanyiwa marekebisho muhimu hivi sasa kwa mujibu wa matokeo ya majaribio ya mfano wa kwanza. Mara tu mchakato huu utakapokamilika, uzinduzi wa muundo wa pili nao utaanza kushughulikiwa.
Hassan Salarieh vilevile amsema, masuala haya ya teknolojia yanahitaji kurudiwarudiwa na kupitiwa mara kwa mara. Tunatarajia kwamba teknolojia nyingi zitajaribiwa na kuimarishwa katika uzinduzi huo.