
Wakati mashambulii hayo ya Ukraine dhidi ya Urusi yakiarifiwa, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonesha wasiwasi wake kuhusu mashambulizi ya droni yaliyoripotiwa katika mpaka wa nchi yake na Hungary. Kupitia ukurasa wake wa X, Zelensky amesema droni zinazoingia katika anga ya Ukraine zina uwezekano mkubwa kuwa zinatoka Hungary.
Hungary yakanusha droni zake kushambulia Ukraine
Waziri wa mambo ya kigeni wa Hungary Péter Szijjártó, amezijibu tuhuma hizo akisema Zelensky ameanza kuchanganyikiwa na anaanza kuona vitu ambavyo havipo. Ukraine imekuwa ikiikosoa nchi hiyo jirani kwa kile inachokiona kuwa ukaribu na Urusi.