
Kuna wagombea 12 watakaoshiriki katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 12, 2025 nchini Cameroon. Miongoni mwao, Rais anayemaliza muda wake Paul Biya, aliye madarakani tangu mwaka 1982, anawania muhula wa nane akiwa na umri wa miaka 92. Wagombea hao 12 wanawasilishwa hapa kwa mpangilio wa kuonekana kwao kwenye orodha rasmi ya Elecam (Elections Cameroon), chombo kinachohusika na kuandaa uchaguzi.
Imechapishwa:
Dakika 4 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Caxton Ateki Seta, mzaliwa wa Mbengwi, katika eneo linalozngumza Kiingereza lililokumbwa na mgogoro Kaskazini Magharibi, anawakilisha Chama cha Muungano wa Kiliberali (PAL). Akiwa na umri wa miaka 39, huu ni uchaguzi wake wa kwanza wa urais, baada ya taaluma katika mashirika mbalimbali ya kiraia. Yeye ni mmoja wa wagombea wachache waliofanya kampeni huko Bamenda na Buea na anaonyesha wasiwasi kwamba wapiga kura katika maeneo mawili yanayozungumza Kiingereza hawataweza kupiga kura Oktoba 12 kutokana na ukosefu wa usalama. Ameshiriki katika majadiliano na wagombea wengine kwenye jukwaa la makubaliano na anatoa wito wa mabadiliko ya serikali baada ya miaka 43 ya urais wa Biya.
Bello Bouba Maïgari, 78, ni mmoja wa mawaziri wawili kutoka eneo la Kaskazini walioondoka serikalini miezi michache kabla ya uchaguzi wa rais. Akiwa mkuu wa chama cha National Union for Democracy and Progress (UNDP), ambaye hapo awali alikuwa akishirikiana na chama cha rais, CPDM, alitangaza kujiuzulu Jumamosi, Juni 28, baada ya kuhudumu kama Waziri wa Nchi na Utalii kwa miaka 14. Alishiriki katika uchaguzi wa urais wa mwaka 1992. Wakati huo, akitangazwa rasmi kuwa wa tatu, alipinga ushindi wa Paul Biya.
Paul Biya, kama kiongozi wa chama chake cha Cameroon People’s Democratic Movement (CPDM), ndiye mgombea wa uchaguzi wa mwezi Oktoba. Rais anayemaliza muda wake wa Cameroon, akiwa na umri wa miaka 92, anatafuta muhula wa nane mfululizo baada ya miaka 43 ya uongozi wa nchi.
Jacques Bougha-Hagbe, mwanauchumi ambaye alifanya kazi kwa zaidi ya miaka 20 katika IMF. Akiwa na umri wa miaka 50, huu ni uchaguzi wake wa kwanza wa urais, chini ya bendera ya Vuguvugu la Wananchi wa Cameroon (MCNC). Anatoa wito wa kukomeshwa kwa kizazi cha “Ahidjo/Biya”—marais wawili pekee wa Cameroon tangu uhuru mwaka 1960—na pia anashiriki katika majadiliano na wagombea wengine kuhusu mageuzi yanayoweza kutokea siku za usoni. Anatetea marekebisho ya kitaasisi na mfumo mdogo wa rais, usio na serikali kuu, na, kwa upande wa kiuchumi, wa kujiondoa kutoka kwa faranga za CFA na kukuza Eneo Huru la Biashara ya Bara la Afrika (AfCFTA).
Issa Tchiroma Bakary ndiye waziri mwingine, anayetoka eneo la Kaskazini, kujiuzulu kutoka kwa serikali mwezi Juni ili kutangaza kugombea uchaguzi wa urais chini ya bendera ya Cameroon National Salvation Front (CNSF). Amehudumu kama Waziri wa Ajira kwa miaka sita iliyopita. Hapo awali, alikuwa Waziri wa Mawasiliano kwa miaka tisa. Aliteuliwa kuwa “mgombea wa makubaliano” na watu wachache wa kisiasa, bila kupata uungwaji mkono wa wagombea wengine katika kinyang’anyiro hicho. Akiwa na umri wa miaka 79, ili kuelezea kujiuzulu kwake, alisema, miongoni mwa mambo mengine, kwamba hakuwa tena na nafasi ya kumpata Mkuu wa Nchi na kwamba Rais huyo hafai tena kuitawala Cameroon.
Samuel Iyodi Hiram. Akiwa na umri wa miaka 38, mhandisi na kiongozi wa biashara, ndiye mgombea mdogo zaidi katika uchaguzi wa urais. Kama wagombea wengine kadhaa, anatetea muungano wa vikosi vya upinzani kufunga ukurasa wa miaka ya Biya.
Pierre Kwemo ana maisha marefu ya kisiasa nyuma yake. Mzaliwa wa Bafang katika Mkoa wa Magharibi, naibu kiongozi wa zamani wa chama cha Social Democratic Front (SDF), alikuwa meneja wa kampeni ya mwaka 2004 wa Ni John Fru Ndi, mpinzani wa muda mrefu wa Paul Biya aliyefariki mwaka wa 2023. Akiwa na umri wa miaka 69, hii ni mara yake ya kwanza ya kugombea urais, na anawakilisha Muungano wa Harakati za Kisoshalisti (UMS). Akiwa ameshiriki kwa miaka mingi katika jukwaa la urekebishaji wa kanuni za uchaguzi, anashikilia kuwa UMS ni sehemu ya mantiki ya muungano wa mabadiliko.
Cabral Libii Alitangazwa rasmi kuwa wa tatu (6.28%) katika uchaguzi uliopita wa urais mnamo 2018, Cabral Libii ana umri wa miaka 45. Kiongozi huyu wa zamani wa wanafunzi na mwanahabari anawakilisha Chama cha Maridhiano cha Cameroon (PCRN) baada ya vita vya muda mrefu vya kisheria kuwania nafasi ya mkuu wa chama hicho. Mnamo mwaka wa 2017, Cabral Libii alizindua vuguvugu la “Waliosajiliwa Milioni 11” ili kuwahimiza Wacameroon kujiandikisha kupiga kura. Kama wagombea wengine kadhaa wanaompinga Paul Biya, anatoa wito wa ufuatiliaji mkubwa wa raia kwenye vituo vya kupigia kura siku ya uchaguzi.
Serge Espoir Matomba, mjasiriamali na diwani wa manispaa huko Douala, mji mkuu wa kiuchumi wa Cameroon. Huu ni uchaguzi wake wa pili wa urais. Mnamo 2018, alipata rasmi chini ya 1% ya kura. Mwaka huu, akiwa na umri wa miaka 46, chini ya bendera ya People United for Social Renewal (PURS), anatetea kurejeshwa kamili kwa uhuru wa Cameroon.
Akere Muna, mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani Salomon Muna, mzaliwa wa eneo la Momo katika eneo linalozungumza Kiingereza la Kaskazini-Magharibi, alikuwa kiongozi wa chama cha Wanasheria wa Cameroon na rais wa shirika lisilo la kisetikali la Transparency International Cameroon. Mgombea wa chama cha Universary, alihusika katika kesi ya Glencore kushutumu ukosefu wa uchunguzi na mashtaka nchini Cameroon kufuatia kukiri kwa kampuni ya kimataifa ya uchimbaji madini, ambayo ilipatikana na hatia ya hongo iliyolipwa kwa maafisa wakuu nchini Cameroon na nje ya nchi. Mnamo Agosti, ombi lake la kutostahiki dhidi ya Paul Biya lilikataliwa na Baraza la Katiba. Katika hilo, Akere Muna alikemea “hali ya utegemezi” ambayo kwa mujibu wake, mkuu wa nchi anajikuta kutokana na umri na afya yake.
Joshua Osih Asili kutoka eneo la Kusini-magharibi linalozungumza Kiingereza, mwanaharakati katika Social Democratic Front (SDF) kwa miongo mitatu, Joshua Osih alikuwa naibu kiongozi wa Ni John Fru Ndi kabla ya kuwa rais wa chama mwaka wa 2023.