Urusi imerusha “mamia ya ndege zisizo na rubani na makombora” dhidi ya Ukraine usiku wa Jumamosi, Septemba 27, kuamkia Jumapili, Septemba 28, kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andriy Sybiga.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Urusi imeanzisha mashambulizi mengine makubwa ya anga dhidi ya miji ya Ukraine wakati watu wamelala. Kwa mara nyingine tena, mamia ya ndege zisizo na rubani na makombora, yameharibu majengo ya makazi na kusababisha vifo vya raia,” Andriy Sybiga ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Meya wa mji mkuu, Vitali Klitschko, ameripoti majeruhi sita, watano kati yao walilazwa hospitalini baada ya shambulio “kubwa”. Jiji la Zaporizhzhia (kusini-mashariki) limepigwa “angalau mara nne,” kulingana na gavana wa eneo, Ivan Fedorov, ambaye aliripoti majeraha wanne.

Mshauri mkuu wa Rais Zelensky, Andriy Yermak, amezungumzia mashambulizi ya kutumia ndege zisizo na rubani na makombora. 

Wakati huo huo Kyiv inaishutumu Moscow kwa kukata mtambo wa nyuklia wa Enerhodar, mkubwa zaidi barani Ulaya, katika eneo hili na kutaka kuunganisha na gridi ya taifa ya Urusi licha ya hatari za kiusalama. Miundombinu hiyo ilishikiliwa na wanajeshi wa Urusi mnamo mwezi Machi 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *