
Wakati kampeni za uchaguzi mkuu ziking’oa nanga mwishoni mwa juma lililopita nchini Cameroon, kiongozi mkongwe wa taifa hilo Paul Biya anayewania kuchaguliwa kwa muhula wa nane hakuonekana.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa wanadiplomasia walio karibu na ikulu ya Cameroon, wamesema kiongozi huyo alisafiri juma moja lililopita kwa ziara kwenye nchi za Ulaya na kwamba yuko mjini Geneva, bila hata hivyo kueleza ni lini atarejea nyumbani.
Jumla ya wagombea 12 akiwemo Paul Biya, walipitishwa na tume ya uchaguzi kushiriki uchaguzi wa Octoba 12, uchaguzi ambao Biya anapewa nafasi kubwa ya kushinda.
Kutokuwepo nchini mwake kuzindua kampeni za chama chake kumezidi kuibua maswali kuhusu afya yake, miezi kadhaa kupita tangu azushiwe kufariki.
Wapinzani Wake, Cabral Libii wa chama cha upinzani cha National Reconciliation, alizindua kampeni zake kwenye mji wa Douala, huku waziri wa zamani wa utalii Bello Bouba Maigari na mgombea mwingine Akere Muna não wakizundua kampeni zao.
Biya hajawahi kuhutubia raia wa nchi hiyo tangu Julai 13 mwaka huu ambapo aliandika kwenye ukurasa Wake wa kijamii wa X alipotangaza nia ya kugombea kiti cha urais.
Aidha Biya alishindwa kuhudhuria mkutano wa umoja wa Mataifa jijini New York sikuj ya alhamisi na badala yake aliwakilishwa na waziri Wake wa mambo ya nje.
Septemba 17 katika tukio lililovuta hisia, mtoto Wake wakike Brenda Biya, aliwataka raia wa Cameroon kutompigia kura baba yake, kabla ya baadae kufuta ujumbe huo kwenye mtandao Wake wa TikTok na kuomba radhi.