Wizara ya sheria nchini DRC, imetangaza kusitisha kwa muda wa wiki 5, utoaji wa leseni za makanisa, vyeti vya uraia na nyaraka nyingine katika kile imesema ni kujaribu kukabiliana na vitendo vya rushwa kwenye ofisi za uma.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa kutoka wizara ya sheria, hatua hii inalenga kufichua ukiukaji wa sheria ukiwemo ufisadi katika kutoa hati hizo, uwepo wa mtandao usio rasmi unaotumika katika utoaji wa hati ghushi.

Waziri wa sheria Guillaume Ngefa amesema muda wa kukagua mifumo utasaidia kurejesha uwazi, kuboresha viwango vya huduma kwa wananchi na kurejesha imani ya raia katika taasisi hiyo.

Usitishwaji huu unakuja baada ya raia na mashirika ya kiraia kulalamika kuhusu ukiukwaji wa haki na uwepo wa ukiritimba katika utoaji wa huduma kwenye taasisi husika.

Uwepo wa ufisadi umesababisha upatikanaji wa hati hizo kuwa za gharama ya juu na kuwepo kwa msongamano wa watu wanaosaka hati hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *