Guinea imetangaza kuwa itafanya uchaguzi wa urais Desemba 28, uchaguzi wa kwanza tangu Jenerali Mamadi Doumbouya achukue mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2021.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Raia wa Guinea watapiga kura katika uchaguzi wa urais Desemba 28, ambao ni wa kwanza tangu Jenerali Mamadi Doumbouya achukue mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2021, kwa mujibu wa agizo la rais lililosomwa kwenye televisheni ya taifa.

Hii ni hatua muhimu katika kurejea kwa utawala wa kiraia kwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

“Tarehe ya uchaguzi wa urais imepangwa kuwa Jumapili, Desemba 28, 2025, nchi nzima,” kulingana na agizo la rais lililosomwa siku ya Jumamosi jioni kwenye redio ya umma na kituo cha televisheni cha RTG.

Tangazo hili linafuatia uthibitisho wa Mahakama ya Juu siku ya Ijumaa wa matokeo ya kura ya maoni ya katiba ya Septemba 21, ambayo iliungwa mkono na wananchi wa Guinea. Katiba mpya inaongeza muda wa urais kutoka miaka mitano hadi saba, inaruhusu kuchaguliwa tena, kuanzisha Baraza la Seneti lenye thuluthi moja ya wajumbe wake watakaoteuliwa na rais, na kuunda mahakama maalum ya kuwahukumu maafisa wakuu.

Pia inatoa kinga kwa marais wa zamani na, kwa mara ya kwanza, inaruhusu wagombea binafsi kugombea, vifungu ambavyo vimechochea uvumi kuhusu malengo ya kisiasa ya Rais wa mpito Mamadi Doumbouya.

Mamady Doumbouya, afisa wa jeshi la Guinea ambaye ameshikilia ikulu ya rais ya nchi hiyo tangu Septemba 5, 2021, hajatangaza kugombea uchaguzi wa urais wa Desemba.

Chama chake, Baraza la Kitaifa la Mkusanyiko kwa ajili Maendeleo (CNRD), kilimwondoa madarakani Rais wa muda mrefu Alpha Condé mnamo Septemba 5, 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *