
Wiki iliyopita, Shirika la Habari za Kifedha la Msumbiji (GIFim) lilitoa ripoti ya inayotaja mitandao ya ufadhili wa kigaidi kutoka mwaka 2017 hadi mwaka 2024. Kwa miaka minane, eneo la Cabo Delgado kaskazini mwa nchi hiyo limekuwa likishambuliwa na vuguvugu la kijihadi lenye uhusiano na kundi la Islamic State, vuguvugu ambalo linanufaika na usaidizi wa kifedha wa ndani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Gaƫlle Laleix
Takriban Euro milioni 6 katika ufadhili wa ugaidi zimegunduliwa. GiFim imechunguza karibu miamala 3,500 inayotiliwa shaka iliyotambuliwa na taasisi za benki na huduma za kijasusi za kifedha. Ugaidi nchini Msumbiji unafadhiliwa kupitia amana na uondoaji, kwa fedha taslimu na kwa uhamisho, wa “kiasi kidogo,” lakini ambacho, kikichukuliwa pamoja, hukuza ufadhili mkubwa wa kifedha. Kugawanya fedha hizo hufanya iwezekanavyo kudanganya umakini wa taasisi za kifedha. Sekta ya benki, pamoja na sekta ya uhawilishaji pesa kwa njia ya simu, zimeathirika.
Eneo la Cabo Delgado, ambalo ni kitovu cha shughuli za kigaidi nchini Msumbiji, ndilo lililoathiriwa zaidi na operesheni hizi haramu. Lakini operesheni hizi pia zinapatikana katika mikoa ya Zambezia, Nampula, Sofala, na Manica katika nusu ya kaskazini ya nchi, na pia Maputo.
Orodha ya wahusika katika shughuli hizi ni tofauti: watu binafsi wanaoishi kaskazini mwa nchi, biashara ndogo ndogo, lakini pia watumishi wa umma na mashirika yasiyo ya faida. Tangu mwezi Julai, Cabo Delgado imeshuhudia kuongezeka kwa mashambulizi ya kigaidi. Kulingana na Kituo cha Afrika cha Mafunzo ya Kimkakati, karibu watu 350 waliuawa kaskazini mwa nchi mnamo mwaka 2024.