RAIS WA UNGA80: WANAWAKE NA UONGOZI
Rais wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock akifunga mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 30, 2025

UN Photo/Loey Felipe

“Wanawake wengi marais walio hodari, wengi wao wakiwa wa kwanza kwa nchi zao, wote wanatukumbusha kwamba haki za wanawake ni kipimo cha uhuru wa jamii. Ikiwa wanawake hawako huru, hatimaye hakuna mtu atakayekuwa huru. Ikiwa wanawake wako huru, kila mtu atakuwa huru. Ikiwa wanawake hawawakilishwi kwa usawa, au kushiriki kwa usawa katika jamii, uchumi hufanya vibaya. Makadirio fulani yanaonesha kwamba kufunga pengo la kijinsia kutaongeza dola trilioni 7 kwenye pato la dunia. Na maneno machache yaliyoleta makofi kutoka kwa hadhira hii mara nyingi yalikuwa ni ya kutaja uwezekano wa siku zijazo kuwa na Katibu Mkuu mwanamke.”  Annalena Baerbock, Rais wa UNGA80.

Bofya hapa kupata video nzima ya kufungwa kwa Mjadala Mkuu


MALAWI: WANAWAKE NA ULINZI WA AMANI

Agnes Mary Chimbiri-Molande, Mwakilishi wa Kudumu wa Malawi kwenye Umoja wa Mataifa akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Ni muhimu kusisitiza hatua kubwa ambazo Malawi imepiga katika kuhimiza ushiriki wa wanawake katika operesheni za ulinzi wa amani. Malawi  inapenda kwa dhati kupeleka walinda amani wanawake katika majukumu ya kiutendaji, ikitambua uwezo wao wa kipekee wa kuwasiliana na kushughulikia mahitaji na uzoefu mahsusi wa wanawake katika maeneo yenye migogoro. Jitihada hii haiwawezeshi tu wanawake walioko kwenye huduma hiyo, bali pia inaongeza ufanisi wa jumla wa juhudi zetu za ulinzi wa amani kwa kuimarisha uelewa wa kina kuhusu changamoto za kijinsia katika mazingira haya.” Agnes Mary Chimbiri-Molande, Mwakilishi wa Kudumu wa Malawi kwenye Umoja wa Mataifa.

Bofya hapa kupakua nyaraka ya hotuba, sauti, picha na video


BURUNDI: AFRIKA NA KUPUUZWA KWENYE MAAMUZI
Edouard Bizimana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda wa Burundi, akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Photo/Loey Felipe

“Si amani wala haki za binadamu vinaweza kustawi bila haki ya kijamii, bila usawa kati ya mataifa. Ndiyo sababu Burundi inasimama pamoja na washirika wake wa Afrika na inatetea uwakilishi wa haki zaidi wa Afrika katika vyombo vya maamuzi, hasa Baraza la Usalama. Hili ni takwa halali na fanisi. Inawezekanaje bara zima ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa katika maisha na juhudi za Umoja wa Mataifa kupuuzwa? Afrika ndilo bara pekee ambalo kwa zaidi ya miaka 80 halijawahi kuwa na kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.” Edouard Bizimana, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Kimaendeleo wa Burundi.

Bofya hapa kupakua nyaraka ya hotuba, video, picha na sauti


CANADA: MNEPO WA UKRAINE
Anita Anand, Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Photo/Loey Felipe

“Rais Vladmir Putin aliamini kuwa Ukraine ingeanguka ndani ya siku tatu. Miaka mitatu na nusu baadaye, Ukraine bado ipo imara. Mamlaka yake iko salama, watu wake hawajasalimu amri, ujasiri wao haujavunjika. Msimamo wa Canada uko wazi. Rais Putin haruhusiwi kubadilisha mipaka apendavyo. Kuwa na nguvu hakumaanishi kuwa na haki. Ukraine haitarudi nyuma, wala marafiki zake, ikiwemo Canada, hatutofanya hivyo.” Anita Anand, Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada

Pakua hapa nyaraka ya hotuba, picha, sauti na video


ZAMBIA: MAGEUZI YA UN NI MUHIMU
Mulambo Haimbe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatiafa wa Zambia, akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Photo/Loey Felipe

“Tunakiri kuwa Umoja wa Mataifa umekuwa na kasi ndogo katika kuchukua hatua dhidi ya baadhi ya mizozo, jambo ambalo limesababisha migogoro mikubwa ya kibinadamu. Tunakubali pia umuhimu wa mageuzi muhimu na ushirikishwaji wa kweli, hususan kwa bara la Afrika, ambalo sauti yake bado inazimwa. Baada ya miaka 80, tunapaswa kutafakari juu ya hili na maeneo mengine yanayoweza kuboreshwa.” Mulambo Haimbe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Zambia.

Pakua nyaraka, sauti, video na picha


ST. LUCIA – WAPALESTINA SI WATU WA KUFIKIRIKA
Alva R. Baptiste, Waziri wa Mambo ya Nje wa St. Lucia, akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Wapalestina wanapaswa kuwa na taifa lao wenyewe na uanachama kamili katika Umoja wa Mataifa, halikadhalika taifa la Israeli. Njia pekee kwa Israeli kuwa na mipaka salama ni kwa watu wa Palestina kuishi katika taifa lao linalotambuliwa kimataifa, kulingana na haki ya msingi ya kujitawala. Amani katika Mashariki ya Kati inaweza kupatikana tu kupitia hili — si kupitia mabomu, vita, ugaidi, mauaji ya halaiki, wala kujenga makazi haramu.” Alva R. Baptiste, Waziri wa Mambo ya Nje wa St. Lucia.

Bofya hapa kupakua nyaraka  ya hotuba, picha, sauti na video


ERITREA: AFRIKA NA UUZAJI MALIGHAFI NJE
Osman Saleh Mohamed, Waziri wa Mambo ya Nje wa Eritrea, akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Afrika inasalia kuwa bara ambalo malighafi huuzwa nje kwa zile zinazoitwa nchi zenye uchumi ulioendelea kwa bei ndogo, na bidhaa za viwandani zilizokamilika huingizwa kwa bei zilizopandishwa bei sana, ambapo nchi hizi zinasumbuliwa na hasara kubwa katika fursa za ajira, na ambapo rasilimali watu na nguvu kazi ndogo ya wataalamu na wenye ujuzi inatoroshwa kwa sababu ya uhamiaji na uchukuaji wa wataalamu. Bara ambalo  tawala zinazoongoza hutumia hovyo pesa za mkopo lakini kwa ujanja huonesha dalili za maendeleo huku zikilemewa na deni linaloongezeka; zinajihusisha na ufisadi na utumwa wa kisiasa kwa mataifa ya nje, zinasumbuliwa na kuyumba kwa sababu ya mgawanyiko wa ndani na migogoro ya kudumu.” Osman Saleh Mohamed,  Waziri wa Mambo ya Nje wa Eritrea.

Pakua nyaraka ya hotuba, picha, sauti na video hapa


Kwa mujibu wa ratiba iliyochapishwa kwenye wavuti wa Mjadala Mkuu wa UNGA80 orodha ya wazungumzaji wa siku ya leo ambayo ni ya mwisho ya Mjadala Mkuu ni Eritrea, St. Lucia, Zambia, Canada, Burundi, Algeria, Honduras, Nicaragua, Holy See, Korea Kaskazini, Moldova, Malawi, Nepal, Denmark, Benin, Timor Leste.


NUKUU MUHIMU ZA VIONGOZI – SIKU YA TANO 27 SEPTEMBA 2025
UFILIPINO – WATOTO KWENYE MIZOZO
Maria Theresa Lazaro, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufilipino, akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Ni lazima tuongeze juhudi maradufu kushughulikia majanga ya kibinadamu kote ulimwenguni, tukiangalia mizizi yake na kuwekeza katika majawabu ya kudumu. Ni lazima tuwalinde na kuwasaidia watu waliofurushwa makwao nchini Sudan, Syria, Afghanistan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ukanda wa Sahel, warohingya na katika sehemu nyingine nyingi za dunia. Mwezi Juni uliopita, Katibu Mkuu aliripoti zaidi ya matukio 40,000 ya ukiukwaji wa haki dhidi ya watoto katika migogoro ya kivita, ikiwa ndio idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa katika miaka 30. Hili halikubaliki. Watoto wetu wanatudai amani.” –  Maria Theresa Lazaro, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufilipino

Pakua hapa nyaraka ya hotuba, picha, sauti na video


GUINEA – KATIBA MPYA
Amara Camara, Waziri Nchi, Ofisi ya Rais – Guinea, akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Tulitaka kuipatia nchi yetu katiba ambayo inatuakisi na kutuunganisha. Na hivyo tulianzisha mchakato wa mashauriano na ushirikishwaji. Ilichukua muda mrefu, lakini ilikuwa ni lazima kutokana na historia yetu, na tunajivunia kutangaza kutoka mimbari hii kwamba rasimu ya katiba iliyowasilishwa kwa wananchi wa Guinea kupitia kura ya maoni, imepitishwa kwa idadi kubwa. Kuanzia jana, tarehe 26 Septemba 2025, kufuatia kutangazwa kwake na Mkuu wa Nchi, Guinea sasa ina katiba, ikiashiria kurudi kwake kulikotarajiwa kwa muda mrefu kwenye utawala wa kikatiba.” Amara Camara, Waziri Nchi, Ofisi ya Rais – Guinea

Bofya hapa kupakua nyaraka ya hotuba, sauti, video na picha


NIGER- UNYONYAJI WA RASILIMALI
Lamine Zeine Ali Mahaman Waziri Mkuu wa serikali ya mpito Niger akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Hakika, nusu karne ya unyonyaji wa uraniaumu, haujawaletea watu wa Niger chochote isipokuwa umasikini, uchafuzi wa mazingira, uasi, rushwa, na ukiwa, huku ukiwaletea ustawi na uthabiti wafaransa. Zaidi ya hayo, tangu kuingia madarakani kwa Baraza la Kitaifa la Kulinda Nchi (CNSP) na uamuzi wa Niger wa kutumia mamlaka yake kamili juu ya rasilimali zake, serikali ya Ufaransa, kwa mshangao na taharuki, inataka kutupeleka kwenye kesi za madai zisizo na mwisho ili kuzuia uchimbaji  wa madini yetu.”  Lamine Zeine Ali Mahaman Waziri Mkuu wa serikali ya mpito Niger.

Kupata hotuba nzima, picha, video na sauti bofya hapa

INDIA- USAWA UN
Subrahmanyam Jaishankar, Waziri wa Mambo ya Nje wa India akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Photo/Loey Felipe

Kila mwanachama mwenye uwezo wa kufanya dunia kuwa pahala bora zaidi lazima apatiwe fursa ya kufanya hivyo kwa kadri ya uwezo wake, na kwa hilo liweze kufanyika, marekebisho ya mfumo wa ushirikiano wa kimataifa ni lazima. Muongo wa tisa wa Umoja wa Mataifa lazima uwe wa uongozi na matumaini.” Subrahmanyam Jaishankar, Waziri wa Mambo ya Nje wa India.

Pakua nyaraka ya hotuba, picha, sauti na video hapa

MISRI – GAZA
 Badr Ahmed Mohamed Abdelatty, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri

“Tunakataa katakata mipango yoyote ya kuwafukuza kwa nguvu wapalestina. Huu utakuwa uhalifu wa mauaji ya kimbari. Tunasema hili wazi kabisa. Misri si na haitakuwa lango la kufuta hoja ya Palestina. Tutaendelea kuunga mkono ustahimilivu wa wapalestina wanaopinga na  wanaong’ang’ania ardhi yao ya kitaifa. Hatutawahi, kamwe kuwa washirika katika Nakba mpya.” Badr Ahmed Mohamed Abdelatty – Waziri wa Mambo ya Nje na Uhamiaji wa Misri.

Bofya hapa kupata nyaraka, sauti, video na picha za hotuba

ICELAND – KATIBU MKUU MWANAMKE
Thorgerdur Katrín Gunnarsdóttir , Waziri wa Mambo ya Nje wa Iceland akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Hata hivyo, hakuna nchi iliyo kamilifu, na hakuna iliyofikia usawa kamili. Serikali yangu, ambayo inaongozwa na wanawake watatu kwa mara ya kwanza katika historia yake, imejitolea kusukuma maendeleo haya zaidi. Na kuhusiana na mada hiyo, Iceland inatarajia kuona Umoja wa Mataifa hatimaye ukiongozwa na mwanamke wakati Katibu Mkuu atakapochaguliwa na kushika kuingia ofisini.” Thorgerdur Katrín Gunnarsdóttir – Waziri wa Mambo ya Nje wa Iceland.

Bofya hapa kupakua nyaraka ya hotuba, picha, sauti na video

CUBA – USHIRIKIANO WA KITABIBU
Bruno Eduardo Rodríguez Parrilla, Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Photo/Loey Felipe

“Nathibitisha, kwa mara nyingine tena, kwamba Cuba itaheshimu ahadi zake kwa nchi zote ambazo imetia saini mikakati na programu za ushirikiano wa kimatibabu wa nchi mbili, na itaendelea kuwa tayari kuzipanua na serikali zote zilizo tayari kuendeleza ushirikiano kama huo kwa kuzingatia Sheria ya Kimataifa na sheria zao za kitaifa, kwa maslahi ya ustawi wa wananchi wao. Tangu mwaka 1963, madaktari na wataalamu 605,000 wamefanya, miongoni mwa mengine, upasuaji milioni 17 na kusaidia katika uzazi wa watoto zaidi ya milioni 5. Hivi sasa, wataalamu wa afya zaidi ya 24,000 wanatoa huduma zao katika nchi 56.”  Bruno Eduardo Rodríguez Parrilla, Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba.

Pakua nyaraka, hotuba, sauti na video hapa


UJERUMANI – UFADHILI KWA UN
Johann Wadephul, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Ujerumani ni mchangiaji wa pili kwa ukubwa katika mfumo wa Umoja wa Mataifa.
Sisi ni miongoni mwa wahisani wakubwa wa misaada ya kibinadamu kwa Gaza.
Tutaendelea kutoa msaada kupitia washirika waliothibitishwa wanaofanya kazi kwa kuzingatia misingi ya kibinadamu — ukiwemo Umoja wa Mataifa. Msaada huu lazima uwafikie watu wanaouhitaji zaidi. Tunarudia wito wetu wa dharura kwa Israel kuruhusu ufikishaji salama wa misaada ya kibinadamu.” Johann Wadephul, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani.


URUSI – SERA ZA MAGHARIBI

Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Uhalisia wa dunia hivi sasa bado haujaakisiwa ipasavyo katika muundo wa taasisi wa Shirika letu. Jambo la umuhimu ni kulifanyia mageuzi Baraza la Usalama. Urusi inaunga mkono demokrasia ndani ya Baraza kwa kuongeza uwakilishi kutoka Asia, Afrika, na Amerika ya Kusini. Tunaunga mkono maombi ya Brazil na India ya kuwa wanachama wa kudumu katika Baraza hilo, sambamba na kurekebisha dhuluma ya kihistoria dhidi ya Afrika — kwa mujibu wa vigezo vilivyokubaliwa na nchi za Afrika zenyewe.” Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi.

Pakua nyaraka ya hotuba, sauti, video na picha hapa.

SAINT KITTS AND NEVIS – UTETE WA VISIWA VIDOGO
Terrance M. Drew – Waziri Mkuu wa Shirikisho la Saint Kitts na Nevis akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Sisi ni watu ambao hatupimi nyakati kwa miaka pekee, bali kwa dhoruba. Hebu fikiria: Mzee mvuvi, ambaye mikono yake imekauka kama kamba iliyozeeka, akitazama mwamba wa matumbawe uliokuwa ukibeba nyavu zake ukitoweka polepole mpaka hakuna kilichobaki cha kuvua isipokuwa kumbukumbu. Fikiria madarasa yasiyo na paa na nyumba zisizo na maji yanayotiririka. Kwetu sisi, hizi si lugha ya mafumbo; haya ndiyo mashaka yetu kila msimu wa kimbunga unapoingia. Sayansi ya tabianchi ni kali na dalili zake ni mbaya.”   Terrance M. Drew, Waziri Mkuu wa Shirikisho la Saint Kitts na Nevis.

Bofya hapa kupata nyaraka, hotuba, sauti na video

BURKINA FASO – MIPANGO YA NCHI HAINA MJADALA
Rimtalba Jean Emmanuel Ouedraogo – Waziri Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Serikali – Burkina Faso akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Kwa vyovyote vile, Burkina Faso inasisitiza tena kikamilifu kwamba  vipaumbele vyake havina mjadala,  na kwamba kile inachofanya kinapaswa kuheshimiwa zaidi ya wakati wowote ule. Tunaelekeza hatua zetu kwa mujibu wa mshikamano na umoja, tukiwa na imani ya dhati kwamba watu walioshikamana pamoja kwa lengo moja wanaweza kutimiza mambo makubwa. Juhudi za wananchi wetu wa nyumbani na wa ughaibuni, na uungaji mkono wao kwa shauku kubwa,  vinatutia moyo katika usahihi wa maamuzi tuliyofanya chini ya uongozi wa Rais wa Burkiina Faso.” Rimtalba Jean Emmanuel Ouedraogo – Waziri Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Serikali – Burkina Faso

Pakua nyaraka ya hotuba, picha, sauti na video hapa


Kwa mujibu wa ratiba iliyochapishwa kwenye wavuti wa Mjadala Mkuu wa UNGA80 orodha ya wazungumzaji kipindi cha asubuhi; Bahama, Niger, Grenada, Burkina Faso, Saint Kitts na Nevis, Laos, Armenia, Cambodia, Urusi, Cuba, Brunei, Ujerumani, Iceland, India, Misri, Thailand, Belarus, Mauritania na Romania.

Kipindi cha alasiri kitakuwa na: San Marino, Saudi Arabia, Singapore, Oman, Malaysia, Maldives, Tunisia, Guinea, Ufilipino, na Umoja wa Falme za Kiarabu. 


TOGO
Robert Komlan Edo Dussey Waziri wa Mambo ya Nje na Ujumuishi wa Kikanda na Raia wa Togo walio ughaibuni akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Marekebisho ya mundo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na kuipatia Afrika viti vya kudumu, ni lazima kwa ajili ya heshima na haki. Lakini marekebisho haya lazima yaende sambamba na utambuzi kwamba ukosefu wa usawa wa sasa ulimwenguni unatokana na dhuluma za kihistoria. Kukataa kushughulikia dhuluma hizi ni kuendeleza mfumo wa ushirikiano wa kimataifa  usio kamili. Kwa hiyo, marekebisho ya taasisi za kimataifa ambayo yamekuwa yakidaiwa na watu wa Afrika kwa miongo kadhaa, na ambayo yanafanywa kwa msisitizo zaidi na kwa bidii katika nyakati hizi za vurugu kubwa za dunia, lazima yaeleweke kama ombi la fidia kutokana na kutengwa kwa Afrika ndani ya taasisi za kimataifa.”  Robert Dussey – Waziri wa Mambo ya Nje na Ujumuishi wa Kikanda na Raia wa Togo walio ughaibuni.

Bofya hapa kupata nyaraka ya hotuba, picha, video na sauti.


TRINIDAD NA TOBAGO
Kamla Persad-Bissessar, Waziri Mkuu wa Trinidad na Tobago akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Kupitia uhamiaji wa kihalali, watu wanaruhusiwa kuingia kwa sababu wanatimiza vigezo vya kukaribishwa katika jamii iliyopo na kuongeza thamani katika maisha yao wenyewe, pamoja na jamii waliyojiunga nayo kwa ujumla. Uhamiaji haramu hupuuzia taratibu zote za ukaguzi na uwiano na utaishia kusababisha machafuko ya muda mrefu, kwani wahamiaji haramu wengi hawataweza kujumuika katika jamii zilizopo, na hivyo kusababisha ongezeko la umaskini, uhalifu, na uhasama wa kitamaduni. Hii si hofu wala majungu; ni ukweli mtupu. Nchi ndogo kama Trinidad na Tobago pia inaathiriwa vibaya na uhamiaji haramu.”  — Kamla Persad-Bissessar, Waziri Mkuu wa Trinidad na Tobago.

Bofya hapa kupata nyaraka, hotuba, picha na video.


MALI
Abdoulaye Maïga , Waziri Mkuu wa Mali akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Tofauti na baadhi ya mataifa ambayo yamefungua njia za kupitia kwenye ardhi yao kwa ajili ya magaidi kwa lengo la kushambulia nchi zingine, au kutoa ardhi yao kama kituo operesheni za kificho za wageni, waasisi wa Muungano wa Nchi za Sahel (AES)  kwa kujitolea kwao kwa maslahi ya Afrika nzima, na kwa nia ya kulinda maslahi ya wananchi wao, wameamua kulinda nchi zao huku wakiepuka kuenea kwa tishio katika nchi zingine za Afrika, au hata duniani kote. Kwa kufanya hivyo, wanafanya kazi halisi ya usalama wa umma wa kikanda na kimataifa,”  Abdoulaye Maïga, Waziri Mkuu wa Mali.

Bofya hapa kupakua nyaraka ya hotuba, sauti, picha na video.


LESOTHO
Samuel Ntsokoane Matekane,, Waziri wa Ufalme wa Lesotho akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

Tunakaribisha kwa moyo mkunjufu pendekezo la kuanzisha Vituo vya Kikanda vya Utafiti wa Kilimo chini ya Mpango Kazi wa Awaza kwa nch zisizo na bandari, (LLDCs) ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Vituo vya aina hii vina uwezo wa kutoa fursa ya kupata mbinu na ubunifu endelevu wa kilimo ambazo ni muhimu katika kuimarisha usalama wa kilimo na kupunguza umaskini.Nina furaha kuthibitisha tena nia ya Lesotho ya kuwa mwenyeji wa kituo kama hicho kwa Kanda ya Afrika.”  — Samuel Ntsokoane Matekane, Waziri Mkuu wa Ufalme wa Lesotho.

Bofya hapa kupata nyaraka ya hotuba, sauti, video na picha


BARBADOS
Mia Amor Mottley, Waziri wa Mkuu wa Barbados akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Mkasa halisi wa vita ni kwamba watoto hawa watakapokuwa babu au bibi,  bado wataendelea kujibu maswali yasiyo na hatia yatakayoulizwa na wajukuu zao miaka 70, 80 kuanzia sasa kuhusu jinsi walivyopoteza viungo vyao vya mwili. ‘Bibi/Babu, ulikatwaje mguu wako?’ Na wanapojibu, tunahatarisha kuruhusu vurugu na chuki kuendelezwa kwa vizazi vingine viwili au vitatu. Hii si sababu inayotuleta pamoja. Hili si jambo jema. Na Mheshimiwa Rais hili linafanyika tukiangalia. Tunaweza na lazima tufanye vizuri zaidi ili kudumisha amani kote ulimwenguni kwa ajili ya watoto.” – Mia Amor Mottley,  Waziri Mkuu wa Barbados

Bofya hapa kupata nyaraka ya hotuba, sauti na video.


BANGLADESH
Muhammad Yunus, Mshauri Mkuu wa Serikali ya muda Bangladesh akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Photo/Loey Felipe

“Maendeleo haya Bangladesh hayangewezekana bila mchango wa kipekee wa wafanyakazi wetu wahamiaji. Mwezi baada ya mwezi, wanatuma kiasi kikubwa cha pesa nyumbani  kwao kutokana na kazi yao ngumu wakiwa ughaibuni. Mchango wao si muhimu tu kwa Bangladesh, bali pia una thamani sawa kwa nchi zinazowakaribisha, ambako wanatoa huduma muhimu zinazohitajika sana. Kwa hivyo, uhamiaji una faida kwa pande zote: ni mzuri kwetu, na ni mzuri kwao.”  – Muhammad Yunus, Mshauri Mkuu wa Serikali ya muda Bangladesh.

Bofya hapa kupakua nyaraka ya hotuba, sauti, picha na video.


PAKISTANI
Waziri Mkuu wa Pakistani, Shehbaz Sharif akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

UN Photo/Loey Felipe

“Unawezaje kutarajia nchi inayoendelea na inayokabiliwa na changamoto kubwa za mafuriko kila mwaka kutokana na mabadiliko ya tabianchi, ambalo si kosa letu, na bado tunaambiwa kukopa mikopo mingi zaidi? Nadhani kukopa mikopo kutaharibu uchumi wetu. Tutakuwa bora zaidi tusipokopa mikopo na kusimama kwa miguu yetu wenyewe, kufanya kazi kwa bidii, bila kuchoka, kwa jasho na damu, na kwa neema ya Mungu tutaifanya Pakistan kuwa taifa kubwa.” – Muhammad Shehbaz Sharif, Waziri Mkuu wa Pakistani.

Bofya hapa kupakua nyaraka ya hotuba, sauti, picha na video.


ISRAELI
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

UN Photo/Loey Felipe

“Viongozi wa kiaarabu na waislamu wenye mtazamo wa mbele wanajua kwamba kushirikiana na Israel kutawapatia teknolojia za Israel za kusisimua, ikiwemo katika dawa na sayansi, katika kilimo na maji, katika ulinzi na akili mnemba, na katika nyanja nyingine nyingi. Naamini kwamba katika miaka ijayo, Mashariki ya Kati itaonekana tofauti kabisa. Wengi wa wale wanaoanzisha vita dhidi ya Israel leo watakuwa kesho wametoweka. Wasongesha amani wenye ujasiri watachukua nafasi yao. – Benjamin Netanyahu – Waziri Mkuu wa Israel.

Bofya hapa kupakua nyaraka ya hotuba, sauti, video na picha.


Kwa mujibu wa ratiba iliyochapishwa kwenye wavuti wa Mjadala Mkuu wa UNGA80 orodha ya wazungumzaji kipindi cha asubuhi; Israel, Pakistan, China, Saint Vincent na renadines, Luxembourg, Ireland, Greece, Malta, Bangladesh, Bhutan, Barbados, Solomon Island, Papua New Guinea, -Jamaica, Belize.

Kipindi cha alasiri kitakuwa na: Lesotho, Cabo Verde, Bulgaria, Mali, Andorra, Trinidad na Tobago, Antigua, Fiji, Tuvalu na Tonga, Venezuela, New Zealand,Bahrain, Côte d’Ivoire, Zimbabawe, Mauritius, Vanuatu, Togo.


NUKUU MUHIMU ZA VIONGOZI – SIKU YA TATU 25 SEPTEMBA 2025


RWANDA
Olivier Nduhungirehe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Rwanda inasikitishwa na siasa kuingizwa katika ushirikiano wa maendeleo, jambo ambalo linatumiwa na baadhi ya washirika wa maendeleo kwa sababu na maslahi ya kisiasa ya upande mmoja. Niruhusuni nikumbushe kwamba kila taifa lina mamlaka kamili ya kujitawala na haliwezi kulazimishwa kuchagua kati ya usalama wake na maendeleo yake. Msaada wa maendeleo unapaswa kuwa chombo cha mshikamano na maendeleo, si silaha ya kulazimisha au kushinikiza.– Olivier  Nduhungirehe – Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa – Rwanda


TANZANIA
Makamu wa Rais wa Tanzania Philip Mpango

UN Photo/Cia Pak

“Amani si zawadi ya ziada, bali ni sharti la msingi kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Hivyo basi, ni lazima tuitafute na kuifuatilia amani bila kuchoka. Tunapongeza juhudi za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, viongozi wa dunia, na mashirika yanayojihusisha na upatanisho na utatuzi wa migogoro katika nchi na maeneo kama Mashariki mwa DRC, Sudan, Urusi, Ukraine, na Mashariki ya Kati.”  – Philip Mpango – Makamu wa Rais wa Tanzania

Soma zaidi hapa


DOMINICA
Sylvanie Burton, Rais wa Jumuiya ya Madola ya Dominica akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN.

UN Webcast

“Simulizi ya Miji Miwili ilionesha jamii ambapo wenye nguvu wanaishi kwa starehe na waliotengwa wanateseka kimya kimya. Tunaweza kuzingatia onyo tunalopata kutoka kitabu hicho cha Dickens, kwamba ukosefu wa haki haupaswi kupuuzwa, kwamba wakati mataifa yenye nguvu yanapotumia mamlaka yao juu ya mataifa dhaifu bila kuwajibika au kuzingatia utawala wa sheria, wanapanda mbegu za mgawanyiko na machafuko ya baadaye.”  Sylvanie Burton, Rais wa Jumuiya ya Madola ya Dominica


GHANA
Dramani Mahama, Rais wa Ghana akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN

UN Webcast

“Sasa kila msichana wa Ghana anajua kilele anachoweza kufikia. Maneno ni muhimu, lakini masuala ya uwakilishi ni muhimu zaidi, ndiyo maana Ghana inatarajia kuteuliwa kwa mwanamke kuwa Katibu Mkuu wa taasisi hii siku za usoni. ”  Dramani Mahama – Rais wa Ghana


PALESTINA
Mahmoud Abbas, Rais wa Taifa la Palestina akihutubia kwa njia ya video, Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa

“Tulitambua haki ya Israel kuwepo mwaka 1988 na tena mwaka 1993, na bado tunatambua. Hivyo ni haki taifa la Palestina likatambuliwa pia. Vile vile Ukanda wa Gaza utaendelea kuwa sehemu ya Taifa la Palestina na tuko tayari kuwajibika kikamilifu kwenye uongozi na usalama wa eneo hilo. Hamas hawatokuwa na jukumu lolote kwennye utawala.” Mahmoud Abbas – Rais wa Palestina.

Soma zaidi hapa.


SOMALIA
Hassan Sheikh Mohamud, Rais wa Somalia akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN

UN Webcast

“Wakati ambapo hapo awali tulijitahidi kujiuliza ‘Nini ni sahihi’  chini ya sheria ya kimataifa, leo tunashuhudia kwa wazi kuibuka kwa matumizi ya NGUVU ya kitaifa katika kusuluhisha migogoro. Hii ni njia ya giza na ya hatari sana inayotishia utawala wa sheria wa kimataifa tuliokubaliana kwa pamoja kama nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.Hassan Sheikh Mohamud, Rais wa Somalia.

Soma zaidi hapa


Kwa mujibu wa ratiba iliyochapishwa kwenye wavuti wa Mjadala Mkuu wa UNGA80 orodha ya wazungumzaji kipindi cha asubuhi; Somalia, Montenegro, Palestina, Yemen, Macedonia Kaskazini, Haiti, Georgia, Bolivia, Gabon, Ghana, Guinea-Bissau, Eswatini, . Bosnia na Herzegovina, Palau, Azerbaijan, Equatorial Guinea, na Sudan Kusini.

Kipindi cha alasiri kitakuwa na: Libya, Botswana, Dominica, Micronesia, Ethiopia, Muungano wa Ulaya, Tanzania, Gambia, Uganda, Uholanzi, Ubelgiji, Chad, Sudan, Sao Tome na Principe 


NUKUU MUHIMU ZA VIONGOZI – SIKU YA PILI 24 SEPTEMBA 2025

NAMIBIA
Netumbo Nandi-Ndaitwah, Rais wa Namibia akihutubia akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN

UN Webcast

“Hebu tukumbuke kwamba hata mataifa madogo yana sauti. Pindi sauti zao zinapopazwa na kusikilizwa, amani na haki ya kudumu vita vitatamalaki. Tuna wajibu wa kufanya zama hizo kuwa si wakati wa kutokomea bali wakati wa kuibuka upya. Tuna fursaya kurejesha matumaini na kujenga mustakabali unaoainishwa sio kwa mgawanyiko bali kwa umoja na kuhifadhi utu wa binadamu.”  Netumbo Nandi-Ndaitwah – Rais wa Namibia

Soma zaidi hapa


COMORO
Azali Assoumani, Rais wa Comoro akihutubia akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN

UN Webcast

“Napenda kurejelea azimio lililopitishwa na Baraza Kuu katika kikao chake cha 26 lililotangaza Bahari ya Hindi kuwa eneo la amani, lisilo na silaha za nyuklia na kambi za kijeshi. Hata hivyo, hata leo, tamaa za washindani zinatishia utulivu huu. Kwa hivyo, ninashutumu vikali na kulaani mradi wowote wa kujenga kambi ya kijeshi huko Mayotte, kisiwa cha Comoro ambacho, kwa bahati mbaya, bado kiko chini ya utawala wa Ufaransa.”  Azali Assoumani – Rais wa Comoro

Soma zaidi hapa


SIERRA LEONE
Julius Maada Bio, Rais wa Sierra Leone akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la UN, Septemba 24, 2025.

UN Webcast

Uzoefu wetu unathibitisha ukweli ulio wazi: amani ya kudumu inahitaji ushirikishwaji, umiliki na uhalali. Ukosefu wa usawa wa kimuundo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unadhoofisha uaminifu wake na lazima ushughulikiwe ili kuhakikisha usalama wa pamoja unalindwa.”  Julius Maada Bio – Rais wa Sierra Leone.

Soma hotuba nzima hapa


KENYA
Rais William Ruto wa Kenya akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

UN Webcast

“Leo, tumekusanyika kwa ajili ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa. Swali haliwezi kuepukwa. Je, Umoja wa Mataifa unafaa kwa mahitaji ya wakati wetu? Je, unaweza kuendelea kutumikia binadamu katika mazingira halisi ya sasa? Au umekuwa tu mabaki ya enzi zilizopita?” William Samuel Ruto – Rais wa Kenya

Soma habari nzima hapa


UKRAINE
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha themanini cha Baraza Kuu.

UN Photo/Loey Felipe

“Ili kulinda maisha, Ukraine inajenga shule na hospitali za chini ya ardhi. Ili kulinda maisha, tunalazimika kutumia fedha nyingi zaidi katika kulinda vituo vya umeme kutokana na mashambulizi ya droni na makombora kuliko kujenga vituo vya michezo au miundombinu ya kitamaduni. Wakulima wa Ukraine wanajifunza jinsi ya kulinda vifaa vyao dhidi ya mashambulizi ya droni yanayofanywa na Urusi, na kwao, changamoto hiyo ni kubwa zaidi kuliko mabadiliko ya tabianchi.”  Volodymyr Zelenskyy – Rais wa Ukraine


Mfalme Don Felipe VI wa Hispania akihutubia Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la UN 24 Septemba 2025

UN Webcast

“Kuongezeka kwa idadi ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanaotambua Taifa la Palestina ambapo Hispania iliongeza sauti yake mwezi Mei mwaka huu, lazima kuchangie katika kufikia amani ya kikanda ya haki na ya kudumu inayotokana na utekelezaji wa maazimio ya Umoja wa Mataifa na kwa kutambuliwa ulimwenguni kote kwa Taifa la Israel.” Mfalme  Don Felipe VI wa Hispania


Rais Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akihutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la UN mkutaon wa 80

UN Webcast

“Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC haisaki kuhurumiwa wala salamu za rambirambi, tunataka haki itendeke na jamii ya kimataifa itambue kuwa kinachoendelea Mashariki ya nchi ni mauaji ya halaiki. Umoja wa Mataifa uanzishe tume huru ya uchunguzi na ipatiwe fedha za kutosha. » Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo – Rais wa DRC

Rais João Manuel Gonçalves Lourenço wa Angola akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la UN mkutano wa 80.

UN Webcast

“Dunia imesimama mbele ya uchaguzi wa kufanya kila kitu ili kulinda amani au kukabiliana na vita na madhara yake yote, hivyo kuhatarisha mustakabali wa ubinadamu. Watu wa Palestina hawawezi kulinganishwa na Hamas, kwa kuwa hakuna watu magaidi,’ sembuse watoto magaidi”

Soma habari nzima hapa

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akihutubia mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA79

UN Photo/Loey Felipe

“Tunatengeneza silaha wakati tunapaswa kujenga miundombinu ya kijamii inayoboresha maisha ya watu wetu. Tunapigana vita vinavyosababisha vifo na uharibifu wakati tunapaswa kupambana na umasikini na kuboresha maisha ya watu walioko katika mazingira hatarishi. Lazima tuchukue hatua madhubuti kunyamazisha bunduki zote kila mahali ili kufanikisha Maendeleo Endelevu.” Cyril Ramaphosa – Rais wa Afrika Kusini

Soma taarifa nzima hapa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia ufunguzi wa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 jijini New York, Marekani 23 Septemba 2025

UN Photo/Loey Felipe

“Ukatili haudhibitiwi, halikadhalika ukwepaji wa sheria. Ukwepaji wa sheria ni kama ugonjwa wa kuambukiza, ukikaribisha machafuko, Unachochea ugaidi, na unaongeza hatari ya matumizi holela ya silaha za nyuklia. Uwajibikaji unapopungua, makaburi huongezeka.” António Guterres – Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Soma taarifa nzima hapa

Rais wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock akihutubia ufunguzi wa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la UN (UNGA80)

UN Photo/Loey Felipe

“Uchaguzi ujao wa Katibu Mkuu anayefuata ni kipimo kingine cha uaminifu wa Umoja wa Mataifa, akibainisha kuwa taasisi hiyo haijawahi kumteua mwanamke. Utashtuka kuona, kati ya wagombea bilioni nne, hakuna mmoja aliyetegemewa?” Annalena Baerbock –  Rais wa UNGA80

Soma taarifa nzima hapa

Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu.

UN Photo/Loey Felipe

“Vipaumbele vya jumuiya ya kimataifa ni lazima vigeukie kupunguza matumizi ya silaha, kuongeza misaada ya maendeleo, kupunguza madeni kwa nchi maskini zaidi na kuweka ushuru wa chini duniani ili matajiri wengi walipe ushuru zaidi kuliko wafanyakazi.” Luiz Inácio Lula da SilvaRais wa Brazil 

Soma taarifa nzima hapa

Rais Donald Trump wa Marekani akihutubia Mjadala Mkuu wa UNGA80 New York, Marekani, 23 Septemba 2025

UN Photo/Loey Felipe

“Zama za wahalifu kukimbilia Marekani zimekoma. Tusaidie watu kule kwenye nchi zao kutatua matatizo yao badala ya kuja kwenye nchi yetu na kusababisha matatizo. Watu hawa wanalipa huruma yetu kwa uhalifu.” Donald Trump – Rais wa Marekani.

Soma taarifa nzima hapa.

Fuata ratiba hapa ufahamu kiongozi wako atazungumza lini na saa ngapi.

Tutaendelea kukujulisha yanayojiri na hotuba zinazotolewa kupitia hapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *