Suluhisho la mzozo wa Gaza lipo karibu kufikiwaSuluhisho la mzozo wa Gaza lipo karibu kufikiwa

Johann Wadephul, ameyasema hayo wakati Rais wa Marekani Donald Trump akitarajiwa kukutana hii leo mjini Washington na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kujadili pendekezo la mpango wa amani wa Gaza.

Katika mkutano na mawaziri wenzake wa mambo ya nchi za nje wa Poland, Ufaransa na Ukraine, Wadephul ametoa wito kwa Israel na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas wakubaliane na mpango wa amani wa Trump. Amesisitiza kwamba lazima vita vikomeshwe na mateka wanaoshikiliwa na Hamas warejeshwe nyumbani mara moja.

Tayari Rais Donald Trump akiwa amekwishakutana na Benjamin Netanyahu na muda wowote kutoka sasa watafanya mkutano wa pamoja na vyombo vya habari. Trump alitarajiwa kumshawishi Netanyahu kukubali mpango wake wa amani aliyoupendekeza baada ya miaka miwili ya vita katika Ukanda wa Gaza.

Trump amesema mpango huo unaojumuisha pia kuachiwa mateka na kuwapokonya Hamas silaha ni kama umeshapita baada ya mazungumzo yake wiki iliyopita na viongozi wa nchi za kiarabu na kiislamu. Katika mpango huo Israel nayo pia itatakiwa kuwaachia maelfu ya wafungwa wa kipalestina inaowashikilia wakiwemo wale waliopewa vifungo vya muda mrefu.

Hata hivyo haijajulikana wazi iwapo Netanyahu ataukubali mpango huo kutokana na hotuba yake kali aliyoitoa katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita, akiapa kumaliza kazi aliyoianza dhidi ya wanamgambo wa Hamas na vile vile kukataa katakata mpango wa kuitambua Palestina kama dola huru, kama yalivyofanya mataifa kadhaa ya Magharibi, ikiwemo Uingereza, Ufaransa na Canada.

Smotrich asema israel itaendelea na mapambano yake dhidi ya Hamas

Bezalel Smotrich
Waziri wa fedha wa Israel Bezalel SmotrichPicha: Debbie Hill/UPI Photo via Newscom/picture alliance

Huku hayo yakiarifiwa waziri wa fedha wa Israel Bezalel Smotrich, amesema jeshi la nchi yake litaendelea na mapambano yake dhidi ya Hamas na pia amesisitiza kwamba mamlaka katika ukingo wa Magharibi haipaswi kuwa na jukumu lolote kwa Gaza ya siku za usoni ikiwa ni moja ya mambo yanayoleta mvutano katika mpango wa amani uliopendekezwa na Trump. Mamlaka ya Palestina ndio iliyoisimamia Gaza hadi Hamas ilipochukua madaraka 2007.

Kwengineko Slovenia ambae ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya na mwanachama pia wa Jumuiya yakujihami NATO imempiga marufuku Netanyahu kuingia nchini mwake. Slovenia imesema hatua yake imetokana na Netanyahu kukabiliwa na makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu wa kibinaadamu na mahakama ya kimataifa ya haki pia kugundua kuwa sera nyingi za Israel na matendo yake zinakiuka sheria ya kimataifa na sheria ya haki za binaadamu.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Slovenia amesema kwa kumpiga marufuku Netanyahu kuingia nchini humo kunatoa ujumbe wa wazi kwamba Slovenia inahitaji kuheshimiwa kwa mahakama ya kimataifa na sheria ya haki za binaadamu. Mwezi Julai mwaka huu, Slovenia ilikuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kuwatangaza mawaziri wawili wa Israel wanaotokea mrengo wa siasa kali za kulia, Waziri wa usalama wa taifa Itamar Ben-Gvir na waziri wa fedha Bezalel Smotrich kutoingia nchini humo.

Afrika inasimama wapi juu ya utaifa wa Palestina?

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *