Mwezi mmoja kabla ya uchaguzi wa rais, upinzani unashutumu demokrasia ya ngazi mbili. Kikiwa kimekataliwa mara mbili katika kinyang’anyiro cha urais, ACT-Wazalendo, chama cha tatu kwa ukubwa nchini humo, sasa kinaelekeza matumaini yake yote Zanzibar, visiwa vilivyo na uhuru wa nusu na ngome ya mwisho ambapo upinzani bado unaweza kufanya kampeni.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baada ya Tundu Lissu, rais wa chama cha Chadema kufunguliwa mashitaka, sasa mgombea wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, amekataliwa—licha ya Mahakama Kuu kutoa uamuzi wa kutaka apewe haki zake za kisiasa kwa kugombea katika uchaguzi huo. Ismail Jussa, msemaji wa chama hicho, anakemea jambo hilo na kusema ni ujanja wa kisiasa. “Rais Samia Suluhu Hassan na mgombea urais wa CCM Zanzibar, Hussein Mwinyi, waliteuliwa bila kufuata kanuni. Lakini uteuzi wetu uliyoheshimu kanuni zote za ndani ulikataliwa.” Tunaona huu kama ujanja uliopangwa kundamiza upinzani na kuruhusu chama tawala kutawala peke yake, bila uwajibikaji.”

Kihistoria, upinzani siku zote umekuwa na nguvu Zanzibar kuliko Tanzania bara. Mara nyingi umekuwa ukishindana kwa karibu na chama tawala na tayari umeshiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa. Lakini hata huko, anaonya mtafiti Nicodemus Minde, upinzani unakabiliwa na vikwazo. “Katiba ya sasa haiangazii hali ambayo upinzani unaweza kushinda, kwa sababu rais wa Zanzibar ni sehemu muhimu ya baraza la mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo haifikiriki kwamba anaweza kutoka upinzani.”

Kwa vikwazo hivi kunaongezwa kura ya mapema, siku moja kabla ya uchaguzi wa Oktoba 29, iliyotengwa kwa ajili ya vikosi vya usalama na maafisa wa uchaguzi. Upinzani unaona huu kama mlango ulio wazi wa udanganyifu. Katika safu iliyochapishwa wiki hii, ACT-Wazalendo inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufuatilia kwa karibu uchaguzi wa Zanzibar, mahali pekee, kwa mujibu wake, ambapo “matakwa ya raia bado yanaweza kuheshimiwa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *