
Miaka minane baada ya kuachiliwa kutoka gerezani na miaka mitatu baada ya kupata talaka yake kutoka kwa Laurent Gbagbo, Simone Ehivet sasa analenga kuchukua wadhifa wa juu zaidi nchini Côte d’Ivoire.
Imechapishwa:
Dakika 4 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Simone Ehivet, 79, alizaliwa mnamo Juni 20, 1946, huko Moossou, karibu na eneo la mapumziko la bahari la Grand-Bassam (kusini-mashariki mwa Côte d’Ivoire), ni mtoto wa mwisho kati ya watoto kumi na watano katika familia yao. Akimpoteza mama yake akiwa na umri wa miaka 5, alilelewa na babake, askari. Baada ya shule ya msingi huko Moossou, Bouaké (katikati), na Béoumi (katikati ), alipata shahada yake mnamo mwaka wa 1970 katika shule ya Lycée Classique huko Abidjan.
Akiwa na shauku ya fasihi, alipata shahada nyingine katika Chuo Kikuu cha Abidjan, kilichopewa jina la Félix Houphouët Boigny, mwaka wa 2012. Simone Ehivet kisha akapata mafunzo katika chuo cha École Normale Supérieure d’Abidjan. Kazi yake ya kitaaluma kisha ilimpeleka Paris-XIII, nchini Ufaransa, ambako alipata shahada ya uzamili, na kisha hadi Dakar, Senegal, ambako alipata shahada ya udaktari wa lugha ya ngoma mwaka wa 1981.
Kutoka ualimu hadi mapambano ya kisiasa
nchini Côte d’Ivoire, Simone Ehivet alikua mwalimu wa shule ya upili na akajihusisha na harakati za vyama vya wafanyakazi. Hatimaye aliongoza moja ya vyama hivyo: chama cha walimu wa chuo kikuu. Lakini siasa ilichukua nafasi haraka. Mnamo mwaka 1982, chini ya utawala wa chama kimoja cha Félix Houphouët-Boigny, alianzisha kwa siri chama cha Ivorian Popular Front (FPI) pamoja na wanaharakati wengine, akiwemo Laurent Gbagbo, ambaye alifunga naye ndoa mwaka 1989.
“Alikuwa mwanaharakati aliyejitolea,” anakumbusha Pascal Affi N’Guessan. “Alikuwa mmoja wa wale walioratibu na kutangaza sera za FPI kwa siri wakati Laurent Gbagbo akiwa uhamishoni,” anaongeza kiongozi wa sasa wa chama cha Ivorian Popular Front.
Baada ya jaribio la awali lililoshindwa mwaka 1990 na ujio wa siasa za vyama vingi, Simone Ehivet alichaguliwa kuwa Mbunge wa Abobo, Abidjan, mwaka wa 1995 na kuongoza kundi la wabunge wa FPI. “Nimekuwa nikimfuata tangu miaka ya 1990 nilipokuwa mwanafunzi mdogo,” anasema Bénédicte Konan, ambaye sasa ni mwanachama mkuu wa Movement of Capable Generations (MGC), chama cha Simone Ehivet. “Yeye ndiye aliyenitia moyo kujihusisha na siasa. Aliweza kujiimarisha katika mazingira yaliyotawaliwa na wanaume,” anongeza mwanaharakati huu.
Kuanzia Ikulu ya rais hadi jela
Mnamo mwaka 2000, wakati Laurent Gbagbo alipoingia madarakani baada ya kumshinda Jenerali Robert Gueï, Simone Ehivet alikua mke wa rais. Mwanamke mwenye ushawishi mkubwa, alichukua jukumu kuu katika kuhamasisha wanaharakati wa ngazi ya chini, hasa katika kukabiliana na uasi uliozuka mwaka wa 2002. Kabla ya FPI kuondoka madarakani, alikuwa msimamizi wa mikakati ya kisiasa kwa shule ya chama. Kwa wafuasi wake, yeye ni mpiganaji wa upinzani ambaye anapinga shinikizo kutoka kwa waasi, Ufaransa, na jumuiya ya kimataifa. Wakati huo, wapinzani wake walimshtaki kwa kila uovu.
Uchaguzi wa 2010 na mgogoro uliofuata baada ya uchaguzi ulivuruga kazi yake. Akiwa amejifungia pamoja na mumewe katika chumba cha chini cha makazi ya rais katika kitongoji cha Cocody, alikamatwa pamoja naye Aprili 11, 2011. Laurent Gbagbo alihamishwa hadi Korhogo (kaskazini) na kisha Uholanzi. Simone alizuiliwa huko Odienné, kaskazini-magharibi mwa Côte d’Ivoire. Alihukumiwa mwaka wa 2016 hadi miaka 20 jela kwa “kuhatarisha usalama wa serikali,” alipewa msamaha mnamo 2018 na Alassane Ouattara, kufuatai maridhiano ya kitaifa. “Pamoja na magumu yote aliyovumilia, alipotoka gerezani, hakuacha vita na imani yake. Alisimama imara. Hilo ndilo lililonivutia kuhusu yeye,” anasema Franck Kouassi, mratibu wa MGC kanda ya Gbèkè.
Ukurasa mpya wa kisiasa
Baada ya kuachiliwa kwake, Simone Ehivet alitalakiana na mumewe Laurent Gbagbo, aliyeachiliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na ambaye alionekana hadharani pamoja na mwanamke mwingine, Nady Bamba. Talaka hiyo ilikamilishwa mnamo mwaka 2023 na mahakama ya Abidjan. Utengano wa kibinafsi lakini pia wa kisiasa: Simone Ehivet alianzisha Vuguvugu la Able Generations (MGC) mnamo Agosti 2022, akidai kutaka kujumuisha njia mbadala.
Lakini ni nguvu gani ya kweli ya chama hiki kipya? Kulingana na Dk. Edie Guipié, mwanasayansi wa siasa, “ni vigumu kutathmini uzito wa kisiasa wa chama hiki kwa vile hakijashiriki uchaguzi.” Mchambuzi huyu anaonyesha, hata hivyo, kwamba “wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, MGC ilishinda nafasi tano za madiwani wa manispaa kutokana na ushirikiano wake.” Anahitimisha: “Uchaguzi wa urais utakuwa mtihani halisi kwa chama hiki changa.”
Kuidhinisha kwa Baraza la Katiba kugombea kwa mke wa rais wa zamani kumezua matumaini mapya miongoni mwa wafuasi wake. “Siku zote tumekuwa na wanaume kwenye uongozi wa nchi hii. Kwa nini asijaribu mwanamke?” anauliza mwanaharakati mmoja. Anaongeza, “Simone Ehivet ana ujuzi wa kuongoza Côte d’Ivoire.”