
Nchini Uganda, kampeni za urais za Januari 12, 2026, zinaanza leo Jumatatu, Septemba 29. Rais wa sasa Yoweri Museveni, 81, anawania muhula wa saba baada ya takriban miaka arobaini madarakani. Mpinzani wake mkuu, mwanamuziki aliyegeuka kuwa mpinzani Bobi Wine, anajumuisha matumaini ya vijana waliokata tamaa lakini walio wengi. Ni mazingira kama yale ya mwaka 2021, lakini hali ya kisiasa imekuwa ngumu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Yoweri Museveni anaangazia rekodi yake. Baada ya takriban miaka arobaini madarakani, rais anaahidi kuendelea “kulinda amani na ustawi wa Uganda.”
Mpinzani wake, Bobi Wine, anaangazia uundaji wa nafasi za kazi, elimu bora, na vita dhidi ya ufisadi, ujumbe ambao unawagusa vijana waliokatishwa tamaa.
Lakini mazingira ambayo kampeni hii inafanyika inasalia kuwa isiyo ya haki, kulingana na upinzani. Tume ya Uchaguzi, iliyoteuliwa kabisa na rais, inasalia mikononi mwa serikali, na tangu uchaguzi uliopita, zaidi ya wanaharakati 300 kutoka chama cha Bobi Wine wamekamatwa, wengine wakifikishwa mbele ya mahakama za kijeshi.
Halafu kuna Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa rais na mkuu wa majeshi. Katika mitandao ya kijamii, ametoa kauli nyingi za uchochezi: vitisho dhidi ya wapinzani, mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya Bobi Wine na mgombea wa zamani Kizza Besigye, ambaye bado yuko gerezani.
Mahakama ya Juu iliagiza mnamo mwezi Januari 2025 kuwa mashtaka ya kijeshi dhidi ya raia yasitishwe, lakini Besigye anaendelea kuzuiliwa.
Kwa mtaalamu wa masuala ya siasa kutoka Uganda Tolit Atiya, anasema “hatari halisi ni idadi ya vijana wenye hasira, wanaomfahamu mkuu mmoja tu wa nchi, ambao wanaweza kuvutwa katika wimbi jipya la vurugu.”
Mnamo mwaka 2021, zaidi ya watu 50 walipoteza maisha wakati wa maandamano kando ya kampeni za uchaguzi uliopita.