Mahakama Kuu ya Kijeshi ya Kinshasa inatarajiwa kutoa uamuzi wake leo Jumanne, Septemba 30, katika kesi inayomkabili rais wa zamani Joseph Kabila. Awali hukumu hiyo ambayio ilipangwa kutolewa Septemba 12,  iliahirishwa kufuatia ombi la vyama vya kiraia, ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini, na Kivu Kusini, wakiomba mijadala katika kesi hiyo ifunguliwe.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika kikao cha awali, Kiongozi mkuu wa Mahakama Kuu ya Kijeshi, Joseph Mutombo, alithibitisha uamuzi huu, na kufufua kesi nyeti ya kisheria yenye athari kubwa za kisiasa.

Hukumu ya kifo imeombwa

Upande wa mashtaka, ukiwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Lucien René Likulia, umeomba adhabu ya kifo kwa Joseph Kabila kwa uhaini, uhalifu wa kivita, kuandaa uasi na kula njama. Unamtuhumu kiongozi huyo wa zamani wa nchi kuwa mchochezi mkuu wa ukatili unaofanywa na waasi wa AFC/M23 mashariki mwa nchi.

Mashtaka hayo ni pamoja na mauaji, ubakaji, uhamisho na uharibifu, na kusababisha madhara makubwa kwa Jamhuri, kwa mujibu wa upande wa mashtaka. Mbali na adhabu ya kifo, upande wa mashtaka unaomba:

  • Miaka 20 jela kwa kuunga mkono uhalifu wa kivita,
  • miaka 15 jela kwa kula njama,
  • Kukamatwa mara moja kwa mshtakiwa,
  • Kunyang’anywa mali zake,
  • Amri ya kulipa gharama na kifungo.
  • Kesi yenye hatari kubwa

Kesi hii, iliyosikilizwa bila ya mtuhumiwa kuwepo mahakamani, inafuatiliwa kwa karibu nchini DRC na nje ya nchi. Wafuasi wa Kabila wanalaani mateso ya kisiasa, huku wafuasi wake wakizungumzia shambulio lililopangwa kwa lengo la kumuondoa mtu mwenye ushawishi mkubwa katika ulingo wa siasa nchini DRC.

Hukumu hiyo, inayotarajiwa leo Jumanne kulingana na Radio Okapi, inaweza kuashiria mabadiliko ya kihistoria katika vyombo vya sheria vya DRC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *