Majira ya baridi yanakaribia kwa kasi na mapigano makali katika ukanda huo ulioharibiwa na vita yanaendelea kusababisha watu kuhama kwa wingi.

“Ni muhimu tupate usitishaji wa mapigano halafu misaada ianze kuingia, siyo tu ili kuzuia njaa kali ambayo inaendelea kusambaa kuelekea kusini, bali pia kuhakikisha kuwa watoto na familia wanapata hifadhi,” amesema Ricardo Pires msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), , wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi.

Pires amesisitiza kuwa kushuka kwa viwango vya joto katika ukanda huo ulioharibiwa kutaleta “changamoto mpya kabisa”, ikiwa ni pamoja na matatizo ya kiafya kwa watoto na familia zao.

Umm Mohammed Al-Masri, alikimbia kutoka Beit Hanoun kusini mwa Ukanda huo, akifanya kazi katika tanuri ya udongo kuoka mikate na kupika chakula kwa ajili ya watu waliokimbia makazi yao ili kusaidia familia yake.

Umm Mohammed Al-Masri, alikimbia kutoka Beit Hanoun kusini mwa Ukanda huo, akifanya kazi katika tanuri ya udongo kuoka mikate na kupika chakula kwa ajili ya watu waliokimbia makazi yao ili kusaidia familia yake.

Mwenendo wa watu kuhama ni mkubwa

Ameeleza pia kuhusu hali ya uhamishaji mkubwa wa watu unaoendelea Gaza, huku operesheni za kijeshi za Israel katika Jiji la Gaza zikiwalazimu watu kukimbia kutoka kaskazini kuelekea kusini. Hali ni mbaya katika makazi ya muda yaliyojaa watu kupita kiasi ya Al-Mawasi, ambayo “hayawezi kabisa kuchukua idadi kubwa ya watu wanaowasili.”

Tunahusika na mamia ya maelfu ya watu, takriban watu 400,000 waliopoteza makazi yao,” amesisitiza.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA), ni takribani asilimia 18 tu ya Ukanda wa Gaza ambayo haiko chini ya amri ya kuhama au ndani ya maeneo ya kijeshi.

Watu waliopoteza makazi wanahitaji hifadhi kwa dharura, na UNICEF ina mahema 11,000 pamoja na maturubai yaliyo tayari kuingizwa Gaza, amesema Pires.

“Hatuwezi kuingiza misaada hiyo… Hii inaonesha tu jinsi hali ya vifaa na uratibu wa misaada ilivyo duni sana,” amesema.

Msaada kidogo waingizwa Gaza

Akiunga mkono hoja hiyo, msemaji wa OCHA Jens Laerke ameeleza kuwa uwezo wa wahudumu wa misaada kusambaza misaada ndani ya Gaza bado ni wa kiwango cha chini.

Baadhi ya misaada imeweza kuingia,  akitaja kuwa majiko ya kijamii yameweza kuongezewa misaada kwa kiwango fulani, na jumla ya milo 660,000 kupikwa na kusambazwa kupitia jikoni 137 kote Gaza siku ya Jumapili iliyopita.

Lakini uwezo wa kufikisha misaada kwa walengwa unategemea wahudumu wa misaada kuruhusiwa kuikusanya na kuipeleka.

Wafanyakazi wa UNRWA wa Jiji la Gaza wanatoa huduma ya utapiamlo katika kituo cha afya huko Gaza.

Wafanyakazi wa UNRWA wa Jiji la Gaza wanatoa huduma ya utapiamlo katika kituo cha afya huko Gaza.

Sintofahamu ya uingizaji wa misaada

“Mara nyingine inawezekana, mara nyingine haiwezekani,” amesema Laerke, pengine ni kwa sababu ya kutopewa ruhusa na upande wa Israeli au kwa sababu nyinginezo.

Umoja wa Mataifa ulitangaza hapo awali kwamba zaidi ya asilimia 40 ya misafara ya kibinadamu siku ya Jumapili iliyohitaji uratibu na jeshi la Israeli zilikataliwa.

“Misaada mingi iliyokuwa imewasili hivi karibuni, ambayo ilichukuliwa, imeporwa kutoka kwenye malori na watu waliokata tamaa na kwa baadhi ya matukio, na makundi yenye silaha,” ameongeza afisa huyo wa OCHA.

Ameita hali ya sasa kuwa “ya machafuko” na kusisitiza umuhimu wa “dhati” wa kuwa na usitishaji mapigano haraka iwezekanavyo ili kuruhusu wahudumu wa misaada kuanza tena operesheni “ya msaada iliyoratibiwa vizuri na yenye vifaa vya kutosha.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *