Mataifa 8 ya kiislamu yametangaza kuunga mkono mpango wa Amani wa rais wa Marekani Donald Trump, kuhusu vita vya Gaza licha ya kuwa baadhi ya wadau wa Palestina kuonesha kutoridhishwa na mpango huo ambao pia umekubaliwa na Israel.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yao ya pamoja mataifa ya Misri, Qatar, Pakistani, Indonesia, Saudi Arabia, Jordan na Falme za Kiarabu, yamesema yanaunga mkono mpango wa Rais Trump, unaotaka kusitishwa kwa vita, kuachiliwa kwa mateka na kuundwa kwa baraza la mpito la uongozi ikiwemo kutumwa kwa kikosi cha kimataifa kusimamia amani huko Gaza.

Akizungumza baada ya kukutana na waziri mkuu Benjamin Netanyahu, rais Trump, amelionya kundi la Hamas dhidi ya kukataa mpango huo aliosema utamaliza vita iliyodumu kwa miongo kadhaa.

Kwa upande wake waziri mkuu Netanyahu, amesema nchi yake inayakubali mapendekezo ya Washington, lakini akaonya kuwa atamaliza alichokianza huko Gaza, ikiwa Hamasa haitaonesha nia ya dhati kumaliza vita.

Mbali na kuungwa mkono na nchi za kiislamu, mataifa ya Ulaya pia yakiongozwa na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, yametangaza kuunga mkono mpango huo, ambao hata hivyo umeacha maswali mengi kuliko majibu hasa kuhusu suala la suluhu ya uwepo wa mataifa mawili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *