
Uwanja wa ndege mkuu wa Israel umesimamisha kwa muda safari za ndege baada ya jeshi la Yemen kufanya operesheni maalumu ya shambulizi kwa kutumia kombora la ‘hypersonic’ aina ya Palestina 2 na ndege zisizo na rubani dhidi ya miji ya Tel Aviv na Eilat ya utawala wa kizayuni wa Israel.
Shirika la utangazaji la Israe (KAN) limeripoti kuwa usafiri wa anga katika uwanja wa Ndege wa Ben Gurion ulisitishwa kwa muda, huku kuruka na kutua kwa ndege kadhaa kukiakhirishwa, zikiwemo safari za ndege za mashirika kya ndege ya El Al, Israir, na Arkia.
makombora yaliyovurumishwa na jeshi la Yemen yalisababisha milio ya ving’ora katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na eneo la kuu la Tel Aviv na katika Uwanda wa Pwani ya Kusini, ambayo ni makazi ya mamilioni ya Waisraili.
Harakati ya Ansarullah ya Yemen imesema kuwa maeneo mengine nyeti ya utawala wa Kizayuni yamelengwa kwa droni mbili huko kusini mwa mji wa Eilat.
Jeshi la Yemen jana lilifanya operesheni hiyo maalumu ya kwa kutumia kombora la ‘hypersonic’ aina ya Palestina 2 na ndege zisizo na rubani dhidi ya miji ya Tel Aviv na Eilat ya utawala wa Kizayuni wa Israel siku tatu baada ya Israel kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya jeshi la Yemen huko Sana’a mji mkuu wa Yemen na kuuwa watu wanane na kuwajeruhi zaidi ya 140.
Ripoti ya Wizara ya Afya ya Gaza inaeleza kuwa Israel imewaua shahidi Wapalestina wasiopungua 66,005 na kujeruhi maelfu ya wengine katika Ukanda wa Gaza wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Yemen Brigedia Yahya Saree amesema kuwa, wataendelea kutekeleza wajibu wao wa kidini, kimaadili na kibinadamu hadi uchokozi dhidi ya Gaza utakapokomeshwa na mzingiro dhidi ya eneo hilo la Palestina utakapoondolewa.